JESHI LA POLISI LAENDESHA MSAKO MKALI KWA WALIOWAUA ASKARI WAWILI

image
Kamanda kova akiongea na waandishi wa habari

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa
Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina
yake ya kuwasaka majambazi waliowavamia ,
kuwaua askari wawili na kumjeruhi mmoja na
kisha kupora bunduki aina ya SMG .
Tukio hilo limetokea tarehe 30 /03/2015
majira ya saa mbili usiku huko barabara ya
Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga
Mkoa wa Pwani . Katika tukio hilo majambazI
wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na
silaha zingine waliwavamia ghafla askari
watatu waliokuwa kazini katika eneo la
kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara
mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga
Mkoa wa Pwani . Majambazi hao
waliwashambulia ghafla askari hao kisha
kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30
ndani ya magazine na kutokomea
kusikojulikana.
Majina ya askari wa Wilaya ya Kipolisi ya
Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo :
1 . D . 2865 SGT FRANCIS,
2 . E.177 CPL MICHAEL,
Askari mwenye namba D 5573 D /SGT ALLY
amejeruhiwa kwa risasi kwenye paja la mguu
wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya
Temeke kwa matibabu. Askari huyu kabla ya
kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi
hayo kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo
aina ya SMG ambayo walishindwa kumpora
hivyo wakatokomea kuelekea porila Vikindu.
Katika oparesheni hiyo , nguvu na mbinu zote
za kipolisi zitatumika ambapo vikosi vya Dar
es Salaam na Pwani vilianza kufanya
oparesheni hiyo mara baada ya tukio ili
kuhakikisha kwamba majambazi hao
wanapatikana haraka iwezekanavyo .
Pamoja na oparesheni hiyo kali inayoendelea ,
Jeshi la Polisi linachunguza ili kubaini kama
tukio hili linaashiria vitendo vya ugaidi au ni
ujambazi wa kutumia silaha .
Natoa wito kwa wananchi wa mikoa ya
Pwani na Dar es Salaam kupitia ( dhana ya
polisi jamii) kushirikiana na Jeshi la Polisi
kwa hali na mali kwa kutoa taarifa sahihi .
IMETOLEWA NA :
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑