FAHAMU KIWANGO KIPYA ANACHOLIPWA DIAMOND KWA SHOW MOJA YA MZIKI HAPA TANZANIA

image

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond
Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa
kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana
ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za
Kitanzania humpati kwenye show yako.
Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa
kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye
mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na
mwimbaji huyo.
Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja
wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji
kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa
na shilingi Milioni 25 za Tanzania).
“Tuna show Marekani show kumi na tano (15),
show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa
hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola
e15,000.” Babu Tale aliiambia Bongo5.
Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha
hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi
(ikiwemo Marekani).
“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola
elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa
ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma
kuwa Diamond anauza dawa za kulevya.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15
mara dola 25,000 ni sawa na $375,000 (Sawa
na shilingi za Tanzania 625,687,500).
Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na
tano za kitanzania.
Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli
kuitwa Dangote wa Bongo Flava.
Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo
hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia
ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue
waongee.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑