ALI KIBA AAHIDI KUWACHEKETUA MASHABIKI WAKE

image
Ali Kiba akiongea na Waandishi wa habari.

MSANII wa kizazi kipya anayetamba na
wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh
‘ Kiba ’ ametamka kuwa amejipanga vya
kutosha anahakikisha anawapagaiwisha
mashabiki wake wataojitokeza katika shoo ya
Mwana Dar Live siku ya Sikukuu ya Pasaka ,
Aprili 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Taifa
wa Burudani , Dar Live , Mbagala jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
katika Hoteli ya The Atriums jijini Dar , Kiba
alisema amejipanga vya kutosha kuhakikisha
anadondosha bonge la burudani kwa
mashabiki wake wataokuja katika shoo hiyo
ambapo siku hiyo ataupiga wimbo huo wa
Chekecha Cheketua kwa kutumia ‘ live ’ bendi.
“Nawaomba mashabiki wangu waje kwa
wingi kwani siku hiyo nimejipanga vya
kutosha kuhakikisha napiga shoo kali
ambayo itawapagawisha watu wote ambao
watakuja ukumbini hapo ambapo nyimbo zote
nitaziimba kwa kutumia vyombo vya
jukwaani ‘ live band ’ .
Naye Mratibu wa Burudani katika Ukumbi
huo wa Dar Live , Abdallah Mrisho ‘ Abby
Cool’ amewataka mashabiki wote wapenda
burudani wasikose kufika katika ukumbi huo
siku hiyo ya Sikukuu ya Pasaka kwani
watapata furaha ya kufika ukumbini hapo .
Pia , Isha Mashauzi na Mashauzi Classic
pamoja na Msaga Sumu na Masai Warriors
watanogesha burudani mbalimbali katika siku
hiyo wakimsindikiza Ali Kiba .
Shoo ya MWANA DAR LIVE inaletwa kwenu
kwa udhamini mkubwa wa VODACOM
TANZANIA , SKYY VODKA , RED BULL , VITA
MALT , VALEUR BRANDY , GRANTS ,
JÄGERMEISTER NA GLOBAL PUBLISHERS
LTD.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑