DIAMOND THE PLATNUMZ ATANGAZA RASMI NDOA YAKE NA WEMA SEPETU

image

KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo
kwa mujibu wa takwimu za mauzo nchini
ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii
wa muziki wa kizazi kipya Diamond
Platinumz ametangaza ndoa na
mchumba wake wa muda mrefu Wema
Sepetu anayosema itafungwa hivi
karibuni. Msanii huyo ghali zaidi nchini
kwa sasa, ametamka hayo
alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani
kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi
Jumatano. Alisema kuna mambo mengi
yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo,
ikiwamo maandalizi kwani amepanga
mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini
kitu kinachofanya kidogo mambo
yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni
mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa
yangu watu wengi wanatamani
waihudhurie,” alisema Diamond. Pia
amesisitiza kwamba ndoa si jambo la
masihara kwani ni tendo la kiimani na
ndio maana amekuwa makini katika
mipango yake. “Nataka kila kitu
kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza
hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,”
aliongeza. “Unajua nilishindwa kufanya
mambo haya haraka kwa sababu wengi
nadhani wangeamini kwamba ninafanya
hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi,
tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea
mambo kama ya Instagram tunataka
tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo
Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi
karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri
waswahili wanasema lazima uvifiche,
hata Mwenyezi Mungu naye anasema
anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu
vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda,
hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana
vinaweza kutofanikiwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑