INAUMA! NJEMBA AKIHARIBU KITOTO CHA MIAKA 3

image

Hii ni laana! Njemba mwenye umri
wa miaka 27 aliyetambuliwa kwa jina
moja la Osward, amekiharibu vibaya
kitoto cha kike (jina linahifadhiwa )
(3 ) baada ya kukiingilia kimwili huko
Yombo Njiapanda ya Mwinyi , jijini
Dar es Salaam Julai 7 mwaka huu .

image
Kitoto cha kike (3 ) kilichoingiliwa
kimwili na njemba mwenye umri wa
miaka 27 kikiwa na mama yake

Habari kutoka eneo la tukio
zinasema , njemba huyo alifanikiwa
kutimiza azma yake ya
kiendawazimu baada ya kufanikiwa
kumrubuni msichana wa kazi
anayeishi na mama wa mtoto huyo,
ambaye alimwachia na kwenda
sokoni kwa ajili ya mahitaji
mbalimbali.
Ilidaiwa kuwa jamaa huyo
alimuomba hausigeli aliyekuwa
akimuogesha binti huyo mdogo
acheze naye pasipo kutambua nia
yake, alimruhusu.
Inadaiwa kuwa hausigeli huyo
alimwacha mtoto huyo chumbani
kwa Osward na kuelekea sokoni
lakini aliporejea, alimuona Osward
akimrudisha akiwa amembeba
mgongoni, kitendo ambacho
kilimshtua kwa kuwa mtoto huyo
alikuwa na uwezo wa kutembea
mwenyewe.
Hausigeli huyo alidai kuwa Osward
alimwambia msichana huyo kuwa
mtoto alikuwa amelala ndipo
alipomchukua na kumpeleka
kitandani.

image
Kitoto kikimunyesha mwanahabari
wa Global mahali kilipofanyiwa
unyama huo , huko Yombo Njiapanda
ya Mwinyi , jijini Dar es Salaam

Katika kipindi chote hicho , inadaiwa
kuwa mama mzazi alikuwa katika
mahudhurio ya kliniki kwa kuwa
alikuwa mjamzito wa miezi 9 .
Akisimulia kwa uchungu, mama wa
mtoto, Agnes Musangeleza ( 35)
alisema alirudi nyumbani akiwa
hajisikii vyema kutokana na hali
aliyokuwa nayo , lakini alishangaa
kumuona mwanaye akiwa hana
furaha jambo ambalo lilimshtua ,
hata hivyo hakulitilia maanani mpaka
asubuhi ya siku iliyofuata ambapo
aliitwa na hausigeli aliyekuwa
akimuogesha na kumuonyesha
michubuko mikubwa kwenye
sehemu zake za siri.
“ Nilishtuka sana na haraka nikaenda
hospitali ili kuchukua vipimo , lakini
nilirudishwa kituo cha polisi
Makangalawe kwa ajili ya fomu ya
PF 3 na nilirudi tena Temeke
Hospitali . Baada ya daktari kumpima
mwanangu vipimo vilionesha kuwa
ameingiliwa sehemu ya mbele na
nyuma ,” alisema mama huyo.

image
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Temeke, Engelbert Kiondo.

Alisema katika hali ya kushangaza ,
baada ya kutoa taarifa Polisi na
mtuhumiwa huyo kukamatwa ,
aliachiwa katika mazingira ya
kutatanisha yanayomfanya aamini
kuwa kulikuwa na vitendo vya
rushwa kwa vile kabla ya
kukamatwa, alimfuata na kutaka
kumpa hela ili wamalizane nyumbani
lakini akakataa .
“ Naumia sana mwanangu kufanyiwa
kitendo hiki , nilikuwa nikisoma tu na
kusikia watu wengine wakifanyiwa
hivyo , halafu kibaya zaidi hakuna
hatua yoyote iliyochukuliwa kwa
mtuhumiwa, yupo uraiani ,” alisema
mama huyo na kusema jalada
lililofunguliwa kituoni Chang ’ ombe
lina namba CHA / RB / 4055/ 2014
KUBAKA .
Waandishi wetu walifika eneo la
tukio na kushangazwa na mtoto
huyo ambaye aliwaongoza hadi
chumba cha mtuhumiwa anayedaiwa
kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.

image
Jalada la kesi hiyo ya ubakaji
lililofunguliwa kituo cha polisi
Chang ’ ombe

Mama huyo aliomba msaada wa
kisheria kutoka kwa taasisi za
kutetea unyanyasaji wa kijinsia na
watu binafsi kwani yeye ana mtoto
mdogo wa wiki moja, hana uwezo na
mumewe yupo Mwanza kikazi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Temeke, Engelbert Kiondo alisema
hajapata taarifa za tukio hilo, lakini
kuhusu kuachiliwa kwa mtuhumiwa
huyo, alisema wananchi wengi
hawafahamu taratibu za kisheria ,
kwani hutaka mtuhumiwa
asionekane uraiani hata kama
amefanya kosa linaloruhusu
kupatiwa dhamana na kuongeza
kuwa kama mama huyo anahisi
hajapata haki yake, basi afike ofisini
kwake ili afuatilie jalada la kesi hiyo.
“ Mtuhumiwa akishakamatwa
anaweza akaachiwa kwa dhamana,
hivyo watu wasidhani ndiyo kaachiwa
huru. Cha msingi wasubiri mpaka
pale kesi hiyo itakapoanza
kusikilizwa kwa kuwa kuna taratibu
za kisheria za kufuata kwanza .
Naomba tu huyo mama aje kwangu
nitaangalia kama kuna walakini
katika jalada lake, ” alisema Kiondo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑