BARUA YA WAZI KWA CHIDY BENZ KUTOKA KWA JOSEPH SHALUWA

image

KWAKO,
Rashid Makwilo ‘ Chid Benz’ . Naamini
utakuwa mzima wa afya njema,
kama ndivyo unajisikiaje ukiwa
mzima wakati kuna wenzako wanalia
na afya zao si nzuri kwa sababu
yako?
Lengo la kukuandikia barua hii ni
kukuweka sawa ingawa nakumbuka
mara kadhaa , waandishi mbalimbali
wenye nia njema na wewe waliwahi
kuandika makala za kukuweka sawa.
Matukio yako ya kupiga watu kila
siku si ya kufumbiwa macho kabisa.
Tena ingekuwa bora ungekuwa
unagombana na wanaume wenzako ,
lakini wewe unaowaonea watoto wa
kike!
Kama una nguvu kwa nini usiombe
pambano na Francis Cheka
akuonyeshe kazi ? Wewe si bondia ?
Ukorofi huchafua status ya mtu .
Inawezekana unajiona mjanja lakini
kumbe unafanya mambo ya kijinga .
Hivi juzi tu , ulimshushia kipondo
Aisha Kibuye , ambaye inaelezwa ni
shabiki wako . Ulimpiga hadi
ukasababisha akawa anazimia kila
wakati. Sitaki kuzungumzia hilo sana
maana ni jambo lililofikishwa mbele
ya mahakama.
Lakini nikuulize, raha yako ya kupiga
wenzako ni nini ? Juzi tena,
umemfuata mwanamuziki
mwenzako , Ray C nyumbani kwake
na kumpiga.
Hao nimewatolea mfano maana ni
matukio yaliyoripotiwa, si ajabu huko
mtaani una matukio kibao ya kupiga
watu. Hivi ni ushamba au jela
inakuita?
Kila kukicha unaleta vurugu na
wasanii wenzako . Umegombana na
wengi kwenye kumbi mbalimbali za
starehe. Ni nini unatafuta ndugu ?
Inatakiwa ujichunguze upya na
ubadilike kabla makubwa
hayajakukuta!
Sijajua kinachokusumbua ni nini! Ni
utoto? Wewe si mtoto , maana una
zaidi ya miaka 18, tena zaidi ya
miaka 25! Utoto wako upo wapi ?
Tuseme labda ushamba ! Lakini
nikifikiria ushamba , pia sikupati
maana wewe ni mtoto wa mjini,
tena uliyezaliwa jijini Dar es Salaam ,
eneo la wajanja wa mji – Ilala .
Ushamba wako unatokea wapi ?
Inawezekana ni ugeni wa ustaa ,
labda hukutarajia kuwa msanii na
ukajulikana, kwa hiyo umefura
kichwa na unajiona unaweza
kupigana au kumpiga yeyote kwa
sababu wewe ni staa. Acha
kujidanganya!
Hakuna aliye juu ya sheria . Amini
maneno yangu na ni vyema kama
utayafanyia kazi mapema ,
vinginevyo utaja nikumbuka ukiwa
nyuma ya nondo . Jela si nzuri ndugu ,
kuwa makini.
Usanii siyo ugomvi . Zinduka ndugu,
dunia imebadilika. Magonjwa mengi ,
watu wanatembea na maradhi yao,
utakuja mpiga mtu ngumi moja,
anaanguka na kukata kauli, anafariki
– utakuwa mgeni wa nani ?
Kama ni wa kusikia utasikia, kama ni
sikio la kufa , basi baki na tabia yako
ya hovyo ila siku yakikikuta
utakumbuka. Ni bora nimekuambia,
kuliko kukuacha ukazidi kupotea !
Wenye lugha yao wanasema:
“ Asiyefunzwa na mamaye ,
ulimwengu utamfunza !” kazi kwako .
Yuleyule,
Mkweli daima,
.. .. . .. .. . .. .. . .. .. . .. .. . .. .. . .
Joseph Shaluwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑