NEY WA MITEGO ATOROKEA CHINA AKIKIMBIA KESI YA KUMTISHIA NDUGU YAKE KUMUUA, SOMA ALICHOKISEMA MDOGO WAKE HAPA

image

Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay
alikuwa akiishi na Shija kwa zaidi
ya miaka mitano nyumbani kwake,
Manzese jijini Dar.
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa
Nay na Shija ulianza zaidi ya miezi
mitatu iliyopita ambapo hivi
karibuni walikuwa maeneo ya
Kijitonyama, Dar, wakipata chakula
cha usiku na marafiki zao wengine
ndipo ghafla dogo akajichanganya
na kujikuta akiropoka neno
lililomuudhi Nay, akapaniki.
Ilisemekana kwamba baada ya
kupaniki, Nay alianza kumfokea
Shija na kutishia kumuua, ambaye
alishindwa kujizuia na kujikuta
akimwaga chozi.
Akaendelea kueleza kuwa hata
baada ya siku hiyo, Nay aliendelea
kumtumia SMS za kutishia kumuua
ambazo bado anazo kama ushahidi
Baada ya kudaka mchongo huo,
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija
ambaye pia ni msanii wa Bongo
Fleva na kumuuliza juu ya
malalamiko hayo, akakiri
kugombana na kaka yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai
kuwa Nay amekuwa akiendelea
kumtishia kumuua jambo
linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Alisema ili kujilinda ndipo
alipoamua kulifikisha suala hilo
kwenye Kituo cha Polisi Kitunda,
Dar anakoishi kwa sasa kisha
kufunguliwa jalada la kesi namba
KT/RB/1178/2014 KUTISHIA KUUA
KWA NJIA YA MTANDAO.
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila
mafanikio lakini kwa mujibu wa
mtu wake wa karibu, baada ya
kujua msala huo ametorokea nchini
China
-GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑