Diamond Anatafutwa China…..Aliyejifanya Dansa Wake Adakwa Na Madawa Ya Kulevya Kama Jack Patrick, Ni Katika Uwanja Uleule Wa Ndege Akiwa Na Shehena Ya Unga

image

STAA wa  muziki wa bongo fleva
nchini, Abdul Nassib “Diamond”
ametakiwa kutokanyaga kabisa
nchini China na kwamba
akitokeza  pua yake nchini humo
asahau  kabisa kurudi uraiani…
Hiyo inafuatia kijana mmoja
mtanzania kukamatwa wiki
iliyopita uwanja wa ndege wa
Macau China na kudai kuwa
yeye ni mcheza shoo wa
mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania….
Habari kutoka Macau China
zinadai kuwa kijana huyo
aliyejulikana kwa jina moja la
Manyota alikamatwa akiwa
kwenye harakati za kuingiza
mzigo huo wa dawa za kulevya
kwa kupitia uwanja wa ndege
wa Macau….
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu
vya habari, inaarifiwa kuwa
Manyota alikamatwa Alhamisi ya
wiki iliyopita katika uwanja
uleule aliokamatwa mtanzania
mwingine Jackline Patrick,
anayesotea rumande mpaka hii
leo huko huko Macau  China…..
Kijana mmoja wa kitanzania
anayefanya shughuli zake huko
China amedai kuwa Manyota
alikamatwa na maofisa wa
usalama wa uwanja wa ndege
na katika utetezi wake alidai
kuwa yeye ni mwanamuziki toka
Afrika  Mashariki…
Mtanzania huyo aliendelea
kudai kuwa, Manyota baada ya
kukamatwa alianza kubabaika
kwa kujifanya mwanamuziki na
baadae akadai kuwa yeye ni
mcheza shoo wa mwanamuziki
Diamond  kutoka Tanzania….
“Alijifanya yeye ni mwanamuziki,
baadae akabadilika na kudai
yeye ni mcheza shoo wa
mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania na kwamba ndani ya
ule mzigo alikuwa hajui kuna
nini zaidi ya kuombwa na
jamaa zake wa Dar awapelekee
nchini China”…Alisema
mtanzania huyo
Inasemekana kuwa, ili
kujiridhisha, maofisa hao wa
usalama wa uwanja wa ndege
walimtaka kijana huyo aoneshe
moja ya kazi zake na yeye
akaishia kuwaonesha moja ya
video za Diamond kupitia
mtandaoni na kumuonesha
mmoja wa wacheza shoo wa
mwanamuziki huyo kuwa ndo
yeye Manyota…
Inasemekana kuwa, pamoja na
utetezi wake huo ambao
unaweza kumuingiza matatani
Diamond,maofisa hao wa
usalama walishndwa kumuelewa
na kumtupa  ndani…..
Mtanzania huyo alihitimisha kwa
kudai kuwa, kutokana na
mazingira yalivyo,ni vyema
mwanamuzi Diamond akawa
makini sana kama atakuwa na
safari za kwenda China kwani
kwa namna moja ama nyingine
jina lake limewekwa kwenye
orodha ya majina machafu na
wanaweza kumkamata kwa lengo
la  kuujua ukweli

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑