MAHAKAMA KUMBURUZA WEMA KORTINI MARA BAADA YA KUONYESHA DHARAU.

image

Mahakama ya mwanzo Kawe jijini
dar es salaam imetoa hati ya
kumkamata miss tanzania 2006
Wema Sepetu kutokana na kile
kinachoelezwa kuwa ni dharau ya
wito wa mahakama hiyo.
Chanzo cha ndani kilichoomba
kuhifadhiwa ya jina kimempasha
mwandishi wetu kuwa hati hiyo
ilitolewa mwishoni mwa wiki
iliyopita baada ya wema kushindwa
kuhudhuria kesi yake iliyopo
mahakamani hapo na bila kutolewa
udhuru wowote.
Aidha imeelezwa kwamba
mahakama hiyo pia imetilia
mashaka udhuru uliotolewa
septemba 30 kwamba wema ni
mgonjwa baada ya kuvuja kwa
picha katika mitandao
zikimuonyesha Wema akila bata
Hong Kong China na mpenzi wake
wa zamani mwanamuziki Diamond.
Wema alitolewa udhuru huo na
kijana aliefahamika kwa jina la
Martini .
Kesi inayomkabili wema katika
mahakama hiyo ni ya kumtukana
matusi ya nguoni pamoja na
kumpiga meneja wa hoteli ya
Mediteranian iliyopo Kawe beach
jijini Dar es salaam bwana Godluck
kayumbu.
Baada ya kupata taarifa hizo
mwandishi wetu alimtafuta
mlalamikaji wa kesi hiyo bwana
Kayumbu na kumuuliza kuhusu hati
iliyotolewa na mahakama ambapo
alithibitisha kuwepo kwa jambo
hilo.
Bwana Kayumbu alisema kuwa
amepewa hati maalum ya
kumkamata wema octoba 30 mwaka
huu ambayo kesi hiyo ilitajwa tena
mahakamani hapo.
Alisema kuwa Wema Sepetu
anaweza kukamatwa muda wowote
kuanzia sasa kwani octoba 30
mwaka huu kesi hiyo ilitajwa tena
mahakama ya Kawe chini ya
mheshimiwa hakimu Ikanda lakini
wema hakutokea na hakuna mtu
yeyote aliyekuja kwaajili ya
kumtolea udhuru.
Kayumbu alibainisha kuwa
mshtakiwa wake wema sepetu
hakuja mahakamani mara mbili
mfululizo kuanzia septemba 30
2013 na kudaiwa kuwa anaumwa
lakini picha zake katika mitandao
zilimuonyesha akitanua hong kong
china na mara ya pili kesi hiyo
ilitajwa octoba 30 2013 ambapo
hakutokea mtu yeyote
anayemuhusu wema katika
mahakama hiyo.
“Kesi ilikuwa ya kwanza kutajwa
lakini nilikuwa peke yangu sasa
nikaamuliwa mimi nipewe hati
maalum ya kumkamata wema
ambapo nilipewa na
nimeshaikabidhi kituo cha polisi
cha kawe kwa utekelezaji maana
naona muda unazidi kwenda na
kesi haiishi,” alisema kayumbu.
Mwandishi wetu alipomtaarifu
bwana kayumbu kuwa octoba 30
Wema Sepetu alikuwa kwenye
msiba baada ya kufiwa na  baba
yake mzazi mzee Isaac Sepetu na
kwamba siku hiyo alikuwa safarini
kwenda zanzibar kwa ajili ya
mazishi ya mzazi wake huyo, bwana
kayumbu alisemaa kuwa suala hilo
halimuhusu kwani hata yeye
amefiwa na wazazi wake.
“Kama kafiwa hata mimi nimefiwa
na baba na mama yangu pia,
kinachotakiwa ni kutii sheria za
nchi ikiwemo mahakama ,kama
alifiwa kwanini asitoe udhuru? sina
mazungumzo tena kinachotakiwa ni
sheria ichukue mkondo wake,
popote atakapopatikana wema ni
lazima akamatwe,” alisema
Godluck.
Wema hakupatikana kwenye simu
ili kuzungumzia jambo hilo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑