MAGAZETI CHOCHEZI SASA KUBANWA ZAIDI

image

SERIKALI leo inatarajiwa
kuwasilisha Muswada wa
Marekebisho ya Sheria
mbalimbali, ambapo pamoja na
mambo mengine , magazeti
yanayochapisha habari za
uchochezi zinazosababisha
uvunjifu wa amani katika jamii ,
yataongezewa adhabu.
Muswada huo utawasilishwa leo
bungeni na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, Frederick Werema,
kuhusu sheria mbalimbali 15 ,
ikiwamo Sheria ya Magazeti ya
Mwaka 1976 na Sheria ya
Filamu na Michezo ya Kuigiza .
Vifungu vinavyofanyiwa
marekebisho ni cha 36 (1 ) na
cha 37 (1 ) b, ambavyo vinahusu
adhabu zinazotolewa kwa
magazeti yanayochapisha
habari za uongo na
zinazosababisha uvunjifu wa
amani katika jamii .
Taarifa kutoka Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba,
Sheria na Utawala , zimeeleza
kuwa Mwanasheria Mkuu
alipokuwa akitoa mapendekezo
ya kufanyiwa marekebisho
kwenye sheria hiyo, aliiambia
Kamati hiyo kuwa adhabu
zinazotolewa kwa magazeti
yanayokiuka maadili ni ndogo,
ikilinganishwa na madhara ya
kosa lenyewe katika jamii .
Hivyo alipendekeza kuongeza
kiwango cha adhabu ya makosa,
ili kuhakikisha vyombo hivyo
vinafuata utaratibu na sheria
inayoviongoza.
Sheria hiyo kwa sasa kabla ya
marekebisho kuletwa bungeni,
kifungu cha 36 ( 1) , kinasomeka ;
“mtu yeyote atakayechapisha
habari za uongo , au za uzushi
au kuchapisha taarifa
itakayosababisha woga na
kuleta uchochezi katika jamii au
kuleta usumbufu , utakaondoa
hali ya amani atakuwa
amepatikana na hatia ya
kutenda kosa na atakabiliwa na
adhabu ya kulipa faini isiyozidi
Sh 150 , 000 .
Au kwenda jela miaka isiyozidi
mitatu au kutumikia adhabu
zote kwa pamoja.” Baada ya
marekebisho
yanayopendekezwa, sheria hiyo
inatarajiwa kuongeza adhabu ya
faini hadi Sh milioni tano .
Kadhalika, kifungu cha 37 ( 1) b
kinachohusu uchochezi kwa
lengo la kusababisha vurugu na
kuharibu mali, wahusika
watakabiliwa na makosa ya
kulipa faini ya Sh milioni tano
au kwenda jela miaka mitatu au
kutumikia adhabu zote kwa
pamoja.
Wadau
Habari za uhakika ambazo
gazeti hili limeambiwa kuhusu
sheria hiyo ni kwamba pamoja
na kuwapo au kusikilizwa maoni
na malalamiko ya wadau wa
habari katika jamii , hakuna
mapendekezo yaliyowasilishwa
rasmi ya wadau yakiomba sheria
hiyo ifanyiwe marekebisho au
kubadilishwa.
“Tunafanya kazi kwa kuzingatia
taratibu na kanuni , na kuna
njia mbili za kufanya
marekebisho ya sheria
mbalimbali, njia ya kwanza ni
kupitia kwa Serikali yenyewe
kuleta marekebisho kwenye
Kamati kuhusu sheria husika
kwa kuzingatia kanuni ya 80
(3 ),” alisema mtoa habari .
Aliongeza njia ya pili ni kwa
mbunge au Kamati , kuwasilisha
au kuleta muswada binafsi kwa
kuzingatia kanuni ya 81 (1 ),
ambayo inaelezea marekebisho
ya sheria husika na kutoa
mapendekezo ya jinsi
unavyotaka uwe.
Alisema kwa njia hizo mbili ,
yaani mbunge, Kamati au
Serikali wanaweza kuwasilisha
mapendekezo ya Muswada,
wakitaka kufutwa kwa sheria
husika na wao kutoa
mapendekezo ya jinsi
wanavyotaka iwe .
Mtoa habari alisema kwa
kuzingatia utaratibu huo,
Serikali imeleta marekebisho ya
sheria hiyo , kwa kile ilichoona
kinapaswa kufanyiwa
marekebisho sasa.
Kwa mujibu wa mtoa habari
huyo, mapendekezo hayo
yatawasilishwa leo baada ya
Serikali kupitia Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kushirikisha Baraza la
Habari Tanzania (MCT ) na Idara
ya Habari ( Maelezo) .
Alifafanua, kwamba tangazo
kupitia vyombo vya habari
lilitolewa kati ya Oktoba 12 hadi
14, mwaka huu, likitaarifu
umma na wadau nchini
kukutana na kamati hiyo, ili
kutoa maoni na mapendekezo
yao kuhusu marekebisho ya
sheria mbalimbali , ikiwamo ya
magazeti .
Hata hivyo, kwa mujibu wa
mtoa habari, pamoja na
tangazo hilo, wadau wa habari
hawakujitokeza kutoa maoni yao
isipokuwa Idara ya Habari
(Maelezo) pekee.
Wanahabari na wadau
mbalimbali nchini wamekuwa
wakilalamikia sheria hiyo ya
magazeti wakitaka ifutiliwe
mbali kwa maelezo kuwa ni
kandamizi.
Sheria hiyo ndiyo imekuwa
ikimruhusu Waziri mwenye
dhamana na habari, kuchukua
hatua kali dhidi ya gazeti
linalokwenda kinyume nayo ,
ikiwa ni pamoja na kulifungia .
Kwa sheria hiyo, hivi sasa gazeti
la kila wiki la MwanaHalisi
linatumikia kifungo cha muda
usiojulikana, huku Mtanzania
ikitumikia kifungo cha siku 90;
na hivi karibuni gazeti la
Mwananchi lilimaliza kifungo
chake cha wiki mbili .
Muswada huo unaotarajiwa
kuwasilishwa leo , huenda nao
ukazua majadiliano makali
miongoni mwa wabunge
kutokana na kwamba huenda
usizungumzie kufutwa kwa
Sheria hiyo ya mwaka 1976,
ambayo pia ilipata kutajwa na
Tume ya Jaji Nyalali kuwa
miongoni mwa sheria
kandamizi.
CHANZO NI HABARI LEO

Mwanasheria Mkuu wa
serikali, Frederick Werema

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑