WEMA AZIMIA MARA TATU

image

MISS Tanzania 2006 -07, Wema
Isaac Sepetu , wikiendi iliyopita
aliingia katika kipindi kigumu
zaidi katika maisha yake, kwa
vile lilikuwa tukio zito kulibeba
baada ya kuzimia mara tatu
ndani ya saa 7 .

image

Wema Isaac Sepetu akiwa na
simanzi baada ya kuondokewa
na baba yake mzazi.
Wema ambaye ni nyota wa
filamu Tanzania , alizingirwa na
maumivu makali , yaliyotokana
na kumpoteza mtu
anayempenda sana, baba yake
mzazi, marehemu Balozi Isaac
Abraham Sepetu .
Balozi Sepetu , alifikwa na mauti
Jumapili iliyopita saa 12
asubuhi, ikiwa ni baada ya
kuugua kwa muda mrefu
maradhi ya kisukari na shinikizo
la damu ambavyo
vilimsababishia kupata ugonjwa
wa kupooza viungo ( kiharusi) .
Mzee huyo aliyewahi kushika
nyadhifa mbalimbali serikalini,
alifikwa na mauti akiwa katika
Hospitali ya TMJ, Mikocheni ,
Dar es Salaam alikokuwa
amelazwa.
Awali , Balozi Sepetu alitolewa
Zanzibar alikokuwa anaishi
baada ya kuzidiwa kisha
akapelekwa TMJ, alipopata
nafuu aliruhusiwa kurejea
nyumbani.
Hata hivyo, aliporuhusiwa
hakurejeshwa Zanzibar , badala
yake alipelekwa kwenye nyumba
yake iliyopo Sinza Mori, jijini
Dar es Salaam ambako
alihudumiwa kwa muda kabla
ya afya yake kubadilika na
kukimbizwa TMJ ambako mauti
yalimfika.

image

Wema akiwa na majonzi
wakati wa msiba wa baba yake
nyumbani kwao Sinza Mori
jijini Dar
WEMA KUZIMIA
Chanzo chetu kilisema : “Wema
bado mdogo, katika maisha
yake hakuwahi kupatwa na
msiba mkubwa kama huu ,
kumpoteza baba yake kipenzi ,
ni jambo zito ndiyo maana
mpaka sasa tunaongea
ameshazimia mara tatu , yaani
anazimia na kurejewa na
fahamu.”
Jumapili saa 7 mchana baada
ya kurejewa na fahamu,
alisema: “Nimeumia sana kwani
huu ni msiba mkubwa kwangu,
Baba yangu alikuwa nguzo
imara katika maisha yangu,
sikuwahi kufikiria kama
ningepata msiba mkubwa kama
huu.
“Taarifa hizi wakati nazipokea
nilijua kama utani lakini yote ni
mipango ya Mungu , inaniuma
sana,” alisema Wema.
WASIFU MFUPI WA MAREHEMU
MZEE SEPETU
Balozi Sepetu aliwahi kuwa
Waziri wa Habari , Utamaduni
na Michezo visiwani Zanzibar ,
vilevile akawa Naibu Waziri wa
Mambo ya Nchi za Nje katika
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania , miaka
ya 1970 wakati wa utawala wa
Awamu ya Kwanza chini ya
Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Mwaka 1982, alteuliwa na
Mwalimu Nyerere kuwa Balozi
wa Tanzania nchini Urusi ,
wadhifa ambao aliendelea
kuushikilia mpaka kipindi cha
Awamu ya Pili chini ya Rais
Alhaj Ali Hassan Mwinyi .
Kati ya mwaka 2001 na 2006,
Balozi Sepetu alichaguliwa
kuwa mbunge katika Bunge la
Afrika Mashariki kwa tiketi ya
CCM, Zanzibar .
Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais
Mstaafu wa Zanzibar , Aman
Abeid Karume kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Mamlaka ya Uwekezaji Vitega
Uchumi visiwani humo ( Zipa) .
Machi 27 , mwaka huu , Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed
Shein alimteua Balozi Sepetu
kuendelea na wadhifa huo wa
Zipa kabla ya mauti
kumchukua.
credit~GPL®

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑