DIAMOND NA WEMA WALIKUTANA HONG KONG BADO NI WAPENZI NA WALA HAWAFANYI MOVIE YOYOTE, SOMA HAPA

image

Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa
‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond
na Wema Sepetu iliyopewa jina na
Diamond, ‘Temptations’ haipo na
kama unaingoja, utaingoja hadi
miguu iingie tumboni. Hakuna
movie.
Diamond na Wema Sepetu
walikuwa wakila bata na kufurahia
kama wapenzi wengine
wanaopendana kwa dhati. Kwa
kuangalia picha tu, ni rahisi mno
kujua penzi zito kati ya wawili
hawa. Picha hizo ni ishara kuwa,
Diamond na Wema hawajawahi
kuachana na Diamond amekuwa
akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu wanasema, kama
hujafanya utafiti hauna haki ya
kuzungumza, hivyo ili kuonesha
kuwa hizi si brabra tu, tumefanya
utafiti kwanza.

image

Wema, Diamond na binamu yake
Romeo wakiwa Hong Kong
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni
kuwa, Diamond na Wema Sepetu
walikutana Hong Kong na sio
Malaysia. Wema alienda huko
takriban wiki tatu zilizopita na
hivyo Diamond alimfuata baada ya
kumaliza show yake ya Malaysia.
Kwa mujibu wa msichana aitwaye
Alice aliyeiambia Bongo5,
Diamond alisafiri kutoka Kuala
Lumpur, Malaysia kwenda Hong
Kong kumfuata Wema kwa ndege
ya kampuni ya Air Asia.
“Nilipanda na Diamond flight
moja from KUL to HKG tena ilikua
ni Air Asia X flight number 567
alipandia KUL-LCC Terminal
nilimuona kwenye lounge direct
nikashangaa anafanya nini huku
na baada kufika HKG sijui hata
alipotelea wapi kumbe haya yote
ndo alikua akiyafuata hongera
zao,” alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema
wamekaa wote kwenye hoteli
moja na mpenzi wake Penny
hakuwa anajua kuhusu hili hadi
picha hizi zilipoanza kuenea na
yeye ameshtuka kama
walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo
zimesambazwa na nani lakini kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali,
kuna uwezekano kuwa picha hizo
zimesambazwa na Wema wenyewe
kwa kusudi la kumuumiza Penny.
Kuna taarifa zimeifikia Bongo5
kuwa, Penny ameumizwa mno na
picha hizo na amekuwa akilia siku
nzima. Hata hivyo binafsi
hatujaweza kuthibitisha taarifa
hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny
azungumzie suala hili zimegonga
mwamba kwakuwa simu yake
haipokelewi.

image

Penny
Hivi karibu kwenye birthday ya
Diamond, Penny alielezea kuwa
uhusiano wake na Diamond ndio
mgumu zaidi katika mahusiano
yote aliyowahi kuwa nayo.
“Not the easiest relationship I’ve
ever had..but its the most
intresting! When I’m down, he
would make me feel on top of the
world, my bestfriend, my
brother, my soulmate, my baby,
my man. My strength, my joy, my
love, Ohhh!!! What else do I gotta
say? I love u, and its been a
blessing to have met you, u
taught me that love is just
Me&You the rest shouldnt matter
or make me loose my sleep, today
I ask God to bless u a million
more times, the sweetest
boyfriend ever!!! Crazie
too..unpredictable mind, through
the ups and downs Im gona hold
you down til God says so..you
have taught me that love
conquers all, that Love is pain,
but the pain is worth the while..I
love you baby,” aliandika Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny
walikuwa marafiki wakubwa lakini
kwa mujibu wao wenyewe, urafiki
wao uliharibika hata kabla ya
wote kufahamiana na Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia
jarida la Mzuka kwenye makala
ambayo haikuwa kutoka. “Mimi
sidhani kama nina uadui naye
personally, sijui yeye na urafiki
hatuna. Let me just say kwamba
sio kwasababu ya Diamond.
Nadhani mimi na yeye tulikuwa
tuna issue zetu nyuma ambazo
hazikuwa resolved so tulikuwa
tuna distance mimi na yeye.
Tulikuwa hatuongei maybe kwa
mwaka labda kama sio miezi
nane, we had our own issues
kwahiyo hatukuwa marafiki vile
tena kama tulivyokuwa zamani. So
mimi kuwa na uadui naye sidhani
kama nina uadui. Mimi am happy
unajua, mimi ndo hivyo mimi
naishi maisha yangu am happy na
nilichonacho am happy with my
man, am happy na watu wangu so
am good mimi sina tatizo naye
kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na
Mzuka aliwahi kuzungumzia
alivyojiskia Diamond kuwa na
uhusiano na Penny, rafiki yake wa
zamani.
“It’s a free world, kila mmoja ana
uhuru wake wa kuishi anavyotaka
yeye. They met, they fall in love
wameanza mapenzi, mtu yoyote
anaweza kufall in love na mtu
yeyote asiwe questioned. Love
doesn’t ask why, haiulizi kwanini,
because alikuwa rafiki yangu then
I can’t NO. Wapendana, I wish
them all the best. Mimi na Penny
si kwamba hatuongei sio sababu
ya hii issue, tuna drama zetu tu
za huko nyuma kwahiyo hii issue
ni muendelezo tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na
Diamond waliwahi kuingia kwenye
‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi
mzito, baada ya Diamond
kumrekodi mpenzi wake huyo wa
zamani alipompigia na kuisambaza
sauti kwenye vyombo vya habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba
Naseeb ni mtu wa aina hiyo
kufanya kitu alichokifanya.
Though nimesema kwamba
nitaacha kama ilivyo na
nisingependa kuiongolea lakini
nilikuwa very disappointed, very
very disappointed,” Wema
aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia
muendelezo wa drama hii kutoka
kwa Malkia na Mfalme wa drama
Tanzania.SOURCE:BONGO5.COM

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑