KABURI LA MTOTO ALIYEFUFUKA LAFUKULIWA, MAKUBWA YATOKEA WAKATI WA UFUKUAJI. SOMA HAPA

image

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida
kaburi ambalo alizikwa mtoto
Shabani Maulidi (15), ambaye
anadaiwa kufariki dunia miaka
mitatu iliyopita na kuonekana
akiwa hai hivi karibuni, jana
lilifukuliwa na viungo vya mwili
wake kukutwa ndani.
Kazi hiyo iliyofanyika chini ya
ulinzi mkali wa polisi pamoja na
Mtafiti wa Ofisi ya Mkemia Mkuu
wa Serikali Mkoa wa Mwanza,
Lucas Ndungulu, ilizua taharuki
kwa umati wa watu waliokuwa
eneo hilo, baada ya nyumba ya
jirani lilipo kaburi hilo, Masanja
Marwa, kubomoka ghafla wakati
ufukuaji huo ukiendelea, huku
mwanamke mmoja ambaye
hakufahamika jina lake mara moja
naye akianguka na kuzirai.
Kwa sasa mtoto huyo ambaye
alionekana hai, amelazwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa
uangalizi wa kitaalamu.
Akizungumza na waandishi wa
habari eneo la tukio, Ndungulu
alisema kuwa wameamua kufukua
kaburi hilo ili kupata sehemu ya
viungo vya mwili kwa ajili ya
vipimo.
“Lengo la kufukua kaburi hili ni
kutaka tupate kiungo chochote
cha mwili wa marehemu ili
tufanye utafiti wa kitaalamu ili
tujue kama ni kweli huyu
anayedaiwa kuwa ni mtoto wao
ndiye,” alisema.
Alisema kuwa ufukuaji huo
umemalizika na kwamba
wamepata baadhi ya viungo vya
mwili wa marehemu na kuchukua
baadhi ya mifupa ya mapaja yote
mawili ambayo itapelekwa katika
hospitali ya rufaa kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa Ndugulu, majibu
ya vipimo hivyo yatatolewa baada
ya wiki mbili kama hakutakuwa na
tatizo lolote la kukatika kwa
umeme.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Wilaya ya Geita,
Adamu Sijaona, alisema kuwa
pamoja na kuchukua viungo
hivyo, pia watachukua damu ya
wazazi na mtoto mwenyewe.
“Tumechukua pia damu ya mama
na baba wa Maulidi mwenyewe ili
tukapime vinasaba (DNA) na kama
alivyosema mtafiti, majibu
yatatoka baada ya wiki mbili,”
alisema.
Akizungumza baada ya kazi ya
ufukuaji kumalizika, baba mzazi
wa mtoto huyo, Maulidi Shabani,
alisema kuwa endapo majibu
yatakuja tofauti au vile
wanavyokusudia, wapo tayari
kuyapokea na kwamba
ikigundulika huyo aliyeonekana ni
Maulidi, pia watampokea na
kuendelea kumtunza.
“Lakini nina imani kuwa huyu
aliyeonekana ni mwanangu
Maulidi kabisa, kwa sababu anazo
alama zote,” alisema mzazi huyo.
Mtoto Maulidi aliyefariki dunia
miaka mitatu iliyopita na
kufanyiwa matanga, alionekana
akiwa hai baada ya kukutana na
mama yake ana kwa ana mapema
wiki hii asubuhi wakati akienda
kwenye shughuli zake za biashara.
Ilidaiwa na wazazi wake kuwa
Maulidi alitoweka ghafla na
kushindwa kurudi nyumbani kwao
Januari mosi 2011, wakati
alipokuwa amewapeleka mbuzi
malishoni na mwili wake
kuonekana baada ya siku tatu
akiwa amefia kwenye kisima cha
maji.
Kwa mujibu wa baba yake,
Maulidi hakurudi nyumbani siku
hiyo, ambapo waliendelea
kumtafuta bila mafanikio na
ndipo baada ya siku tatu
walimkuta akiwa amefia ndani ya
kisima cha maji kilicho maeneo ya
Kijiji cha Nyankumbu, Kitongoji
cha Mwembeni.
Tukio hili ni la tatu kutokea
mkoani hapa ambapo wilayani
Kasamwa, mwanamke aliyefariki
dunia miaka mitano iliyopita
alionekana hai na kutambuliwa na
ndugu yake. Tukio la pili lilitokea
Wilaya ya Chato, wakati kijana
aliyefariki dunia miaka miwili
iliyopita alionekana akiwa hai.
VIA/www.mjengwablog.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑