WEMA , DIAMOND WARUDIANA

WACHUMBA wa zamani, Wema
Sepetu na Nasibu Abdul
‘Diamond’ ndiyo habari ya
mjini kwa sasa, kwamba wawili
hao wamerudiana tena kwa
kasi kupita ile ya mwanzo,
Amani limechimbua.
Habari zinasema wawili hao
walikutana Dubai hivi karibuni
kabla Diamond hajaenda
Malaysia na Wema akiwa njiani
kuelekea Hong Kong , China
ambapo walikula bata kwa
sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa
wameamua kuwa kwenye
uhusiano wa siri na lengo la
kufanya hivyo ni kuhakikisha
mpenzi wa sasa wa msanii
huyo wa Bongo Fleva , Penniel
Mungilwa ‘ Penny’ hajui kitu
chochote.
TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani
ya mitandao ya kijamii hasa
kwenye Instagram , maneno
yenye kuashiria kuwa wawili
hao wapo pamoja tena
yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa
habari hizo, Penny naye
alitupia picha yake akiwa
kitandani na Diamond na
kuandika kuwa waachwe kama
walivyo.
Ndani ya mtandao wa
Instagram yakazuka makundi
mawili, upande wa mawifi wa
Penny, akiwemo Halima
Kimwana na kundi lingine la
mawifi wa upande wa Wema .
Kundi la Wema waliandika
kuwa mwanamke anayependwa
na ndugu wa mume siku zote
mwanamme huwa hampendi
hivyo Wema ni mpenzi sahihi
wa Diamond kwa vile
hapendwi na ndugu kama
Penny.
MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali
isiyotegemewa kwenye akaunti
yake ya Instagram , Wema
alitupia wimbo mpya wa
Diamond uitwao My Number
One na kuweka maoni yake
kwamba anaupenda wimbo
huo.
Wengine waliochangia
walisema Wema ana lake
jambo kwa Penny kwa vile si
jambo jepesi kusifia wimbo wa
mwanamme ambaye alikuwa
mpenzi wake na sasa ana
mwingine anayejulikana , yaani
Penny.
PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti
wimbo huo tu , alikwenda
mbele zaidi kwa kutupia picha
yake yenye pozi tamu na
kuuliza; huyu hapa baby wa
nani huyu ? ( yaani yeye ).
Wengi walimsifia lakini
wengine walifunguka kwa
kusema ni baby wa Diamond,
jambo ambalo Wema
hakulipinga.
PENNY AONGEA NA AMANI
Kufuatia kuenea kwa habari
hizo, Amani lilianza kuwasaka
watu watatu ambao ndiyo
wenye uwezo wa kubainisha
ukweli au uongo wa ishu hiyo
iliyoenea mjini .
Watu hao ni Diamond
mwenyewe, Wema anayedaiwa
kurudiwa na Penny , mpenzi wa
sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa
Penny ambapo alipoulizwa
kuhusu kuwepo kwa madai
hayo alifunguka :
AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi
nimenyetishiwa habari hizo
lakini siamini kama
inawezekana hao watu
wakarudiana.
ASEMA KUNA KUNDI
LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la
watu ambao wapo upande wa
pili (wa Wema ) ndiyo
wanaoeneza hizo habari,
pengine wanataka niamini
kisha nimwache Diamond,
simuachi ng’ o .
ANATAKA USHAHIDI
WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia
kwa kuona picha akiwa na
Irene Uwoya hotelini sembuse
hili la safari hii hata picha
hakuna?”
ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza
Diamond, japo hakusema ni
kweli au uongo ila aliniambia
achana na hizo habari. ”
DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny ,
lilimpigia simu Diamond
ambapo alipokea na kusema
yuko kikaoni na kumtaka
paparazi kupiga baadaye . Hiyo
ilikuwa saa 4 :16 asubuhi ya
juzi.
Saa 7 :11 mchana , Diamond
alipigiwa simu tena lakini
hakupokea. Akatumiwa meseji
ya kumkumbushia , hakujibu .
Akatumiwa meseji yenye madai
ambayo pia hakuijibu.
MAMA WEMA KABLA YA
KUULIZWA AFUNGUKIA
MADAWA YA KULEVYA
Amani liligundua Wema bado
yupo Hong Kong hivyo
liliamua kumpigia simu mama
yake, Bi. Miriam Sepetu ili
kuomba namba ya bintiye ,
lakini kabla ya ombi hali ikawa
hivi:
“We nani , hivi kuna gazeti
moja limeandika eti mwanangu
amekamatwa na madawa ya
kulevya China anasubiri
kunyongwa, ni akina nani
wale, wana akili kweli ?
“Mimi sikubali safari hii,
tutafikishana kwa mwanasheria
wangu.
“Tena ukikutana nao waambie
waache kumzushia mwanangu,
wasimtie mkosi bure,
hajakamatwa yupo salama
kabisa. ”
Mpaka sasa ushahidi wa
kuonesha wapenzi hao wa
zamani kuwa wamerudiana
bado haujawekwa hadharani
http://www.globalpublishers.info/m/blogpost?id=5398006%3ABlogPost%3A2687639

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑