Kipsang avunja rekodi ya Berlin Marathon

image

Mkenya Wilson Kipsang
amevunja rekodi ya dunia ya
mbio za Marathon kwa
kupunguza sekunde 15
aliposhinda mbio za Berlin
mapema jumapili.
Mkimbiaji huyo mwenye umri wa
miaka 31 aliandikisha mda wa saa
mbili dakika tatu na sekunde 23
kuondoa rekodi ya zamani
iliyowekwa na Mkenya mwenzake
Patrick Makau miaka miwili
iliyopita.
Rekodi hiyo iliwekwa katika mji
mkuu wa Ujerumani ambako
Makau alikimbia kwa mda wa saa
2:dakika 03:na sekunde 38.
Wakenya wengine walioshiriki
mbio a Berlin Eliud Kipchoge
alimaliza katika mda wa saa
2:04:05) huku Geoffrey Kipsang
akiweka mda wa saa 2:06:26
katika nafasi ya tatu.
Makau hakushiriki mbio hizi
baada ya kujiondoa wiki mbili
zilizopita kutokana na kuuguza
jeraha la goti.
Wilson alifanya mazowezi akiwa
na nia ya kuvunja rekodi ya
Berlin na moja kwa moja alianza
mbio za leo kwa kudhibiri
uongozi katika hatua ya kilomita
10 za mwisho, akiwaacha
wenzake walioonekana kuishiwa
na pumzi ya kumkimbiza.
Baada ya mbio hizi Kipsanga
alisema,” Nimefurahi sana kwa
ushindi huu na kwa kuvunja
rekodi,”
“nilivutiwa mno na Paul Tergat
wakati akikimbia na kuvunja
rekodi hii miaka kumi iliyopita
katika mashindano haya haya.
Ushindi wa Kipsang unampa
jumla ya ushindi wa saba tangu
aanze kushiriki mashindano ya
marathon mjini Paris,Ufaransa
miaka mitatu iliyopita.
Itakumbukwa kuwa Kipsang
alishinda mbio za marathon za
London mwaka jana na kwenye
michezo ya Olimpiki alimaliza wa
tatu na kujishindia medali ya
fedha mjini London.
Ushindi wa mbio hizi za Berlin ni
wa kwanza mwaka huu. Licha ya
mbio za London kua mojapo ya
mbio muhimu duniani na kwake
aliweza kumaliza wa tano
mapema mwezi Aprili mwaka
huu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑