Kibali cha ICC kumkamata mwandishi Kenya

image

Mahakama ya kimataifa ya
ICC, imetoa kibali cha
kukamatwa kwa raia Mkenya
ambaye anatuhumiwa kwa
kujaribu kuwahonga mashahidi
ili wajiondoe kwenye kesi dhidi
ya Naibu Rais wa Kenya
William Ruto.
Viongozi wa mashtaka walisema
kuwa mshukiwa huyo Walter
Osapiri Barasa ameshtakiwa kwa
makosa matatu ikiwemo kutumia
njia za ufisadi kumshawishi
shahidi mmoja na mkewe kwa
kumlipa shilingi milioni 1.4 au
dola 16,200, ili wajiondoe kama
mashahidi katika kesi hiyo.
Aidha mahakama inasema kuwa
ni juu ya Kenya sasa kumkamata
Barasa.
Kiongozi wa mashtaka Fatou
Bensouda amesema kuwa ana
ushahidi wa kutosha kuonyesha
njama ya Barasa kutaka
kuwahonga mashahidi ili
wajiondoe katika kesi dhidi ya
Ruto.
Bensouda amesema kuwa kuna
mtandao wa watu wanaofanya
kila wawezalo ili kuporomosha
kesi dhidi ya Ruto.
Lakini Barasa ameambia BBC
kuwa yuko tayari kujitetea mbele
ya mahakama hiyo na kuonyesha
kuwa hana hatia.
Naibu Rais Ruto na Rais Kenyatta
wameshtakiwa kwa kupanga na
kuongoza ghasia za baada ya
uchaguzi wa mwaka 2007
ambapo watu 1,200 walifariki.
Mahakama ya kimataifa ya ICC
italazimika kuwa na vikao virefu
zaidi vya kusikiliza kesi dhidi ya
Naibu rais wa Kenya William
Ruto, kwa sababu ya muda
uliopotea kutokana na Ruto
kurejea Kenya kwa dharura.
Jaji anayeongoza kesi hiyo Chile
Eboe-Osuji pia alisema kuwa
mahakama itadurusu uwezekano
wa kusikiliza kesi hiyo Jumatano
siku ambayo wangepumzika ili
kuruhusu kesi nyengine
kusikilizwa ndani ya chumba
hicho.
“kama tunavyojua sote
tumepoteza muda katika kesi hii
kwa sababu ya matukio ambayo
hayangeweza kuepukika. Lazima
tuweze kupata muda huo”,
alisema jaji huyo.
Kesi dhidi ya Ruto iliakhirishwa
Septemba 23 kutokana na
shambulizi la kigaidi nchini Kenya
ambalo liliwau watu zaidi ya
sitini.
Hata hivyo jaji huyo alisisitiza
kuwa kesi hiyo itaakhirishwa kwa
muda ili kutoa nafasi kwa kuanza
kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Rais
Uhuru Kenyatta Novemba tarehe
12 ambaye ni mshitakiwa mwenza
wa William Ruto.
Kesi dhidi ya Ruto na mwenzake
Joshua Sang, iliakhirishwa tarehe
23 Septemba, wakati mahakama
ilipomruhusu Ruto kurejea
Nairobi kushughulikia shambulizi
la kigaidi la Westgate na athari
zake.
Source : BBC

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑