ROSE NDAUKA SASA KUZAA BILA NDOA

image

Staa wa filamu za Bongowood, Rose
Ndauka ambaye ni mjamzito
anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa
mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza
na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke,
Malick Bandawe ambaye ni memba
wa kundi la muziki la TNG alianika
aya za Kurani kuwa katika Dini ya
Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na
mwanamke ambaye ni mjamzito
kwani ni sawa na kufunga ndoa na
watu wawili hivyo anamsubiri
ajifungue kwanza. “Ni kweli
mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito
na anatarajia kujifungua mapema
mwezi wanne, mwakani. “Kuhusu
kufunga naye ndoa kwa sasa ni
ngumu hadi ajifungue kwani kwa
dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya
hivyo lakini atakapojifungua tu
tutafunga ndoa,” alisema Malick.
Malick ambaye hivi sasa anatamba
na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema
kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba
mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi
Mungu Rose ajifungue salama kwani
anampenda kupita maelezo. Baada
ya kuzungumza na Malick, gazeti hili
lilimtafuta mama wa Rose Ndauka,
Batuli kufungukia ishu ya mwanaye
kubeba ujauzito kabla ya ndoa
ambapo aligoma kuzungumza kwani
hakubaliani na suala hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑