AZAM TV KUONYESHA MECHI ZOTE ZA YANGA TV

image

KITUO cha Televisheni cha Azam
kimeahidi kuonyesha mechi za
Yanga zitakazochezwa katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam na zile za ugenini kwa
sababu mkataba unawaruhusu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Angetile Osiah
amethibitisha kuwa Azam TV wapo
huru kuonyesha mechi yoyote ya
Ligi Kuu Bara.
Habari nzuri ni kuwa ving’amuzi
vya Azam TV vitaanza kuuzwa
mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya
mwezi ujao kabla ya mechi kuanza
kuonyeshwa ama Oktoba 5 au
Oktoba 9, mwaka huu.
Habari kutoka Azam TV zinasema
kuwa wataonyesha pia mechi
zinazoihusu Yanga kwa sababu
mkataba unawataka kuonyesha
mechi za Ligi Kuu Bara.
Yanga waligoma kusaini mkataba
wa Azam TV kwa madai kuwa Sh
100 milioni ambazo kila klabu
inapewa ni ndogo sana kwao.
“Mkataba wetu unasema kuwa
tunatakiwa kuonyesha mechi za Ligi
Kuu Bara, kwa hiyo tutaonyesha pia
mechi za nyumbani na ugenini za
Yanga, kwa sababu mkataba wetu
tumesaini na Kamati ya Ligi,”
alisema mmoja ya viongozi wa
Azam TV.
Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu
wa TFF, Osiah alisema Azam TV
wapo huru kuonyesha mechi yoyote
kwa sababu mkataba unawaruhusu.
“Hata kama ni mechi za Yanga iwe
Dar es Salaam au mikoani, Azam TV
wanaruhusiwa kuonyesha,” alisema
Osiah.
Katika hatua nyingine, wataalamu
kutoka Afrika Kusini wanatoa
mafunzo kwa wafanyakazi wa
Azam TV mpaka Oktoba 15, mwaka
huu.
“Hawa wataalamu wameomba kabla
hawajaondoka warushe mechi mbili
laivu kuona kama kuna upungufu
wowote. Na ndiyo maana nadhani
mechi za raundi ya saba za Oktoba
5 au mechi za raundi ya nane za
Oktoba 9, zitaanza kuonyeshwa
moja kwa moja,” alisema mmoja wa
mabosi wa Azam TV.
Alisema wataanza kuonyesha mechi
za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
na mechi za mikoani zitaanza
kuonekana baada ya kuwasili kwa
gari la OB Van ambalo
litashughulika na mechi za mikoani
tu.
Kama Azam TV itaanza kuonyesha
mechi Oktoba 5, ina maana
kwamba wataanza na mechi ya
Simba dhidi ya Ruvu Shooting au
siku inayofuata wanaweza
kuonyesha pia Yanga dhidi ya
Mtibwa. Iwapo mechi hizo
hazitaonyeshwa maana yake mechi
za raundi ya nane zinazoweza
kuonyeshwa ni Azam dhidi ya
Mgambo Oktoba 9, au Simba dhidi
ya Prisons Oktoba 12 na Ashanti
dhidi ya Coastal Union Oktoba 13.
Habari za ndani zinasema
ving’amuzi vya Azam TV vitaanza
kuuzwa wiki ya kwanza ya mwezi
ujao.
CHANZO: GAZETI LA MWANASPOTI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑