Waarabu wamshawishi Mrisho Ngassa

image

Klabu moja ya Qatar inataka
kumsajili Mrisho Ngassa kwa
mkataba wa miaka miwili.
Dar es Salaam. Mabingwa wa soka
wa Tanzania Bara, Yanga wanaweza
kumkosa mshambuliaji wao mahiri
Mrisho Ngassa baada ya klabu moja
ya Qatar kuonyesha nia ya kumsajili
huku mchezaji huyo akikiri
kwamba dau walilomuahidi
linamshawishi.
Habari za uhakika ambazo
Mwananchi ilizipata jana zilisema
kuwa, tayari Ngassa
amekwishafanya mazungumzo na
klabu hiyo ambayo ipo tayari
kuilipa Simba SC milioni 45
anazodaiwa na kuifidia Yanga kwa
kumuuza mchezaji huyo.
Taarifa hizo zimesema kuwa klabu
hiyo inataka kumtumia Ngassa
baada ya usajili wa dirisha
dogo.Ngassa alithibitisha hilo huku
akikataa kutaja jina la timu hiyo
kwa sababu za kisheria za usajili
wa wachezaji na kuogopa adhabu
ya Shirikisho la Soka Kimataifa
(Fifa).
Mchezaji huyo alikiri kuwa timu
hiyo ipo tayari kumpa mkataba wa
miaka miwili na kuzilipa Simba SC
na timu yake ya sasa, Yanga.
Alisema kuwa hatua hiyo imekuja
baada ya kuona suala lake la
kuitumikia Yanga katika Ligi Kuu
ya Tanzania Bara linashika sura
mpya kutokana na mvutano wa
malipo.
Alifafanua kuwa klabu hiyo
imemuahidi donge nono na kuamua
kufuta msimamo wake wa zamani
wa kutaka kucheza soka hapa
nchini kutokana na maslahi
anayopata.
“Maslahi yao mazuri na mazingira
waliyoniahidi kimkataba,
nimevutiwa nao kutokana na
ukweli kuwa suala langu la
kuichezea Yanga limekumbwa na
vipingamizi vingi,” alisema Ngassa.
Alisema kuwa baadhi ya wadau wa
Yanga na marafiki zake wana nia
njema ya kutaka kumlipia fedha
anazodaiwa na Simba, lakini
uongozi wa Yanga bado haujatoa
jibu la sakata hilo.
“Nimemaliza kifungo cha mechi
sita, sasa suala lililobaki ni malipo,
viongozi hawajatoa jibu mpaka
sasa, ” alisema Ngassa.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya
Yanga, Clement Sanga alikiri kuwa
bado hawajailipa Simba fedha
wanazomdai Ngassa kutokana na
majadiliano waliyokuwa nayo.
Sanga alisema kuwa wana uhakika
kuwa Ngassa ambaye anafanya
mazoezi ya nguvu na Yanga,
atacheza Jumamosi dhidi ya timu
ngumu ya Ruvu Shooting.
Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑