STAA WA BIG BROTHER MWISHO MWAPAMBA AELEZEA JINSI ANAVYO BAGULIWA NAMIBIA

image

STAA wa Shindano la Big Brother,
Mwisho Mwampamba, amesikitishwa
na vitendo vya ubaguzi alivyofanyiwa
na Polisi wa nchini Namibia,
anakoishi na mkewe, Meryl
Shikwambane, ambapo walimfuata
kwenye nyumba yake na kumtaka
aondoke nchini humo.
Mwisho ameandika kwenye ukurasa
wake wa mtandao wa kijamii wa
Facebook, akisema nchi hiyo sasa hivi
imekuwa kama Afrika Kusini, ambako
wageni, hasa wenye ngozi ya Kiafrika,
hupata shida ya kuishi kutokana na
kubaguliwa.
“Mimi nimeoa mtu wao na nimezaa
naye mtoto, nashangaa kubaguliwa
na polisi hao, pia inashangaza kuona
wakiwahudumia vyema wageni
kutoka barani Ulaya, lakini sisi
Waafrika wenzao tunabaguliwa,”
alisema Mwampamba.
Mkali huyo ameshangazwa kupewa
hati ya kuishi nchini humo kwa miezi
miwili pekee, wakati ameoa
mwanamke wa nchi hiyo, huku
akipata shida hiyo hata mipakani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑