AGNESS MASOGANGE AAHIDIWA NDOA MARA ATAKAPOTUA BONGO

image

MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu
Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘,
Evance Komu amefungua kinywa
chake na kusema; siku mchumba
wake huyo atakapotia miguu nchini,
wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi) yupo
nchini Afrika Kusini alikokuwa
akikabiliwa na kesi ya madawa ya
kulevya ambapo alifanikiwa kuwa
huru baada ya kulipia faini ya randi
30,000 (shilingi 4,800,000)
aliyoamriwa na Mahakama ya
Kempton.
Akizungumza na gazeti hili hivi
karibuni mara baada ya Masogange
kuachiwa, Evance alisema
anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo
kumalizika na kinachofuata kwenye
uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa
kinachomsukuma afanye uamuzi huo
kwa sasa ni kutokana na jinsi
alivyoguswa na changamoto kubwa
alizopitia mchumba wake hivyo
ameona kuna kila sababu ya kumuoa
kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu
ya kutosha na mimi sioni muda wa
kupoteza tena, akitua tu Bongo
kinachofuata ni ndoa nina imani
itakuwa ndiyo jambo kubwa la
kumfariji na kumpa upendo wa hali
ya juu,” alisema Evance pasipo
kutaja siku ambayo mchumba wake
atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili
Masogange, alishikiliwa na mwenzake
Melisa Edward ambaye naye
aliachiwa huru kwa kukosekana na
hatia.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑