SIMBA KUKICHAPA NA MBEYA CITY

image

Ligi Kuu ya Vodacom ( VPL )
inaingia raundi yake ya tano
kesho (Septemba 21 mwaka
huu) kwa mechi huku vinara
Simba wakiwakaribisha Mbeya
City kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam .
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
utakuwa mwenyeji wa mechi
kati ya Mgambo Shooting Stars
na Rhino Rangers ya Tabora .
Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa
Tanzania Prisons katika
pambano litakalochezwa Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
Nayo Kagera Sugar itakuwa
nyumbani kwenye uwanja wake
wa Kaitaba mjini Bukoba
kuvaana na Ashanti United ya
Dar es Salaam katika mechi
itakayochezeshwa na mwamuzi
Jacob Adongo kutoka Mara .
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko
wa tano keshokutwa (Septemba
22 mwaka huu ) kwa mechi tatu
ambapo Azam na Yanga
zitacheza Uwanja wa Taifa , Dar
es Salaam huku JKT Ruvu
ikikwaruzana na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Azam
Complex.
Ruvu Shooting inayokamata
nafasi ya pili kwenye msimamo
wa ligi itakuwa mgeni wa
Coastal Union katika mechi
itakayopigwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la
Kwanza (FDL ) inaendelea
wikiendi hii kwa mechi kumi na
moja. Kundi A kesho ( Septemba
21 mwaka huu ) kutakuwa na
mechi kati ya Transit Camp na
Green Warriors ( Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam ) ,
Tessema na African Lyon
(Uwanja wa Mabatini ,
Mlandizi) .
Ndanda itacheza na Villa Squad
kwenye Nangwanda Sijaona
mjini Mtwara wakati keshokutwa
(Septembe 22 mwaka huu)
kutakuwa na mechi kati ya
Polisi Dar es Salaam na Friends
Rangers katika Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam .
Kundi B kesho (Septemba 21
mwaka huu) ni Mkamba
Rangers dhidi ya Burkina Faso
kwenye Uwanja wa CCM
Mkamba, na Mlale JKT itakuwa
mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga
kwenye Uwanja wa Majimaji
mjini Songea . Keshokutwa
(Septemba 22 mwaka huu) ni
Majimaji na Kimondo katika
Uwanja wa Majimaji .
Mechi za kundi C kesho
(Septemba 21 mwaka huu) ni
Pamba dhidi ya Polisi Dodoma
(Uwanja wa CCM Kirumba ,
Mwanza), Stand United na
Polisi Tabora ( Uwanja wa
Kambarage, Shinyanga ) na
Kanembwa JKT itacheza na
Mwadui kwenye Uwanja wa
Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa
(Septemba 22 mwaka huu)
Polisi Mara na Toto Africans
zitacheza Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume mjini
Musoma.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑