MNIGERIA ASHINDA SHINDANO LA UREMBO LA KIISILAMU

image

A KIISILAMU
Mwanadada wa Nigeria ndiye
mshindi wa shindano la urembo
kwa wasichana wa kiisilamu mjini
Jakarta Indonesia.
Obabiyi Aishah Ajibola, 21,
alishinda shindano la kimataifa la
wasichana wa kiisilamu kwa jina
Muslimah mwaka 2013 siku ya
Jumatano.
Washindani 20 walishiriki
mashindano hayo kuonyesha
mitindo ya kiisilamu pamoja na
maadili ya kiisilamu wakati wa
mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya
shindano kubwa zaidi la
mwanamke mrembo zaidi
duniani, ambalo limeghadhabisha
makundi ya watu wenye
msimamo mkali nchini Indonesaia
kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya
mashindano hayo, walichaguliwa
kutoka miongoni mwa watu 500
waliochaguliwa kwa kutumia njia
ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa
kushirki kwenye mashindano
ilikuwa kusimulia kisa chako na
ambavyo ulianza kuvalia Hijab au
mtandio, ambacho kilikuwa
kikwazo kwa wote waliotaka
kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh,
Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani
walihitajika kuamuka kwa sala ya
asubuhi na kuswali pamoja huku
wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa
miaka 21, alilia na kusoma aya
kutoka kwa Korani, jina lake
lilipotajwa. Alituzwa dola 2,200,
pamoja na ziara ya mji mtukufu
wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa
nia yake ya kushiriki mashindano
hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia
nzima kuwa dini ya kiisilamu ni
nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi
kwenye televisheni kwa kukataa
kuvua mtandio wake, ndiye
alianzisha shindano hilo miaka
mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la
Agence France-Presse kuwa
walifanya shindano hili siku
chache kabla ya shindano la
kimataifa la mwanamke mrembo
zaidi duniani kuonyesha
wasichana kuwa kuna njia
zengine tofauti ambazo unaweza
kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi
kubwa ya waisilamu duniani.
Chanzo: bbcswahili

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑