RAIS KIKWETE AWASHUKIA WANASIASA

image

Rais Jakaya Kikwete
*Asema hatawatetea wauza
‘unga’
*Ashangazwa na kiwango cha
uongo
RAIS Jakaya Kikwete, amesema
anashangazwa na kiwango cha
uongo cha baadhi ya wanasiasa
ambao hakuwataja majina, kuwa
wamekuwa wakizusha madai
kuwa Rais aliteua wajumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
bila kuongozwa na mapendekezo
ya wadau mbalimbali
waliopendekeza majina hayo.
Alisema bado anaendelea kuamini
mchakato wa Katiba mpya
utafikia mwisho wake mwaka
2014 na hivyo kuiwezesha
Tanzania kufanya uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015, chini ya Katiba
mpya.
Alisema hana tatizo na watu
wanaopinga sera za serikali ama
hata kumpinga yeye binafsi, bali
tatizo lake ni wanasiasa na
wanaharakati wanaochochea
ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.
Rais Kikwete, aliyasema hayo juzi,
mjini San Rafael, California, nchini
Marekani, wakati alipokutana na
kuzungumza na jumuia ya
Watanzania waishio katika Jimbo
la California.
Katika hotuba yake, ambayo
alizungumzia mambo mbalimbali,
Rais Kikwete aligusia mjadala wa
karibuni bungeni kuhusu
mchakato wa Katiba mpya na
kusema kuwa alishangazwa na
madai kuwa yeye kama Rais,
hakuongozwa na mapendekezo ya
wadau wakati anateua Tume ya
Katiba.
“Watu wote niliowateua
walipendekezwa na wadau
mbalimbali, zikiwamo taasisi za
dini. Yule Mama Maria Kashonda
alipendekezwa na Baraza la
Maaskofu Tanzania (TEC), Mama
Mwantumu Malale alipendekeza
na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA). Kila kundi
ambalo lilipendekeza watu
limepata mjumbe katika tume
hiyo, wakiwemo walemavu ambao
naambiwa nimewasahau,” alisema
Rais Kikwete na kuongeza:
Kuhusu kama Tanzania itaweza
kupata Katiba mpya kabla ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,
Rais Kikwete alisema:
“Ningependa sana na kwa kweli
ni matarajio yangu makubwa,
tuweze kumaliza mchakato wetu
mwaka 2014 na tuweza kuwa na
Katiba Mpya ili iongoze Uchaguzi
Mkuu wetu wa mwaka 2015.
Mchakato wetu unakwenda vizuri
na wala siyo lazima tuhangaike na
Katiba kwa miaka mingi. Muhimu
ni ushirikishwaji wa kila mmoja
wetu.”
Akizungumzia tabia za wanasiasa
wa Tanzania kwa jumla, hasa
wale wanaochochea chuki na
ghasia, Rais Kikwete aliwaambia
Watanzania hao:
“Sina tatizo na wanasiasa ama
wanaharakati kupinga sera za
Serikali yangu. Hili ni suala la
nguvu ya hoja na tunao uwezo
mkubwa sana wa kutetea sera
zetu. Na wala sina tatizo na watu
kunipinga mimi binafsi.
Kinachonipa taabu mimi ni pale
wanasiasa na wanaharakati
wanapochochea ghasia na kuleta
fujo. Kama mtu anataka kuongoza
Tanzania si asubiri hadi
atakapochaguliwa?”
Aliongeza Rais Kikwete: “Hivi
unapochochea ghasia, fujo na
chuki na kweli mambo hayo
yakatokea na nchi ikateketea,
utaongoza nchi ya namna gani?
Utaongoza magofu na majivu
yatakayobakia baada ya nchi
kuteketea?”
Kuhusu mjadala wa karibuni
kuhusu kama Rais awe na
madaraka ya kuteua wajumbe 166
wa nyongeza ili kuingia katika
Bunge la Katiba kujadili Rasimu ya
Katiba Mpya, Rais Kikwete
amesema kuwa yeye hana tabu
kama itabidi ateua basi atateua,
lakini kama siyo lazima yeye hana
tabu. MTANZANIA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑