LINA AFUNGUKA JUU YA UHUSIANO WAKE NA AMINI

image

Msanii wa muziki wa bongo fleva
ambaye sasa ni mjasiriamali pia
Anasteria Sanga Linah au muite
Ndege Mnana amefunguka kuwa
producer wa studio ya Bhitz
Pancho Latino ndiye mwenye siri
nzito ya penzi lake na msanii
mwenzake Amini ambaye kwasasa
penzi lao limekuwa stori ya kale
baada ya kuachana. Linah
amesema tokea wanaanza
mapenzi yao Pancho ndiye
alikuwa mtu pekee anayejua
mambo mengi kuwahusu wao na
jinsi walivyotumbukia katika
penzi ambalo anasema yeye
binafsi ndiye hasa alikuwa
akimpenda Amini kupita kiasi
japo baadaye akagundua kuwa
hata mwenzake naye anamzimika
na hivyo penzi likawa linasonga.
“Yaani we muulize Pancho yule
ndio ana siri kubwa sana ya penzi
langu na Amini,yaani jamani
nilimpenda sana Amini mpaka
nikakubali kuingia kwenye
mapenzi na nilimpenda hasa
kutoka moyoni,kuna vitu vingi
nyuma yake ambavyo Pancho
anajua”,alisema Linah.
Msanii huyo mwenye sauti tamu
kiasi cha kupachikwa jina la
Ndege Mnana na msanii mkongwe
Patricia Hillary ameendelea
kufunguka kuwa wakati
ameangukia katika penzi la Amini
alikuwa anawachomolea wanaume
wengi waliokuwa wanamtokea
tena wenye pesa zao na wengine
ni watu wazito lakini aliamua
kutoka moyoni kwa dhati kuwa
na Amini kwahiyo akawa
anamtunzia heshima yake.
Anasema kama angekuwa macho
juu kuna uwezekano mkubwa
asingeendelea kuwa na Amini au
angekuwa anamsaliti kwa kiasi
kikubwa lakini moyo wake usio na
tamaa ndio ulikuwa unamfanya
aendelee kumpatia penzi la kweli.
Akavujisha siri kuwa Amini ndiye
aliyemtibua na ndipo akapitisha
uamuzi wa kujiweka pembeni
kwasababu ambazo ni ngumu
kuziweka hadharani lakini mpenzi
wake huyo wa zamani anazijua na
ni sababu ambazo haziwezi tena
kulirudisha penzi lao japo anakiri
kuwa aligundua kuwa mpenzi
wake huyo wa zamani anampenda
siku alipomtamkia kuwa mapenzi
yameisha kila mmoja ashike lake.
Anasema katika kuonesha kuwa
ameachana na Amini lakini hana
bifu naye wakaamua kutoa wimbo
wa pamoja wa Mtima wange.
Akizungumzia show anazofanya
na Amini jukwaani wakiwa kama
wapenzi anasema ni kuonesha
kuwa hakuna bifu na hata
mabusu anayopigwa na
zilipendwa wake huyo anayapokea
kwasababu anashindwa
kuyapotezea jukwaani akiogopa
kumtia aibu jamaa huyo mbele ya
mashabiki na watu wengine.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑