LIGI KUU BARA:TAMBWE NOMA, SIMBA KILELENI

image

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa
kimataifa wa Burundi, Hamis
Tambwe amefunga mabao manne
akiiongoza Simba kuisambaratisha
Mgambo Shooting kwa mabao 6-0,
huku Yanga wakilazimishwa sare
1-1 na Prisons kwenye Uwanja wa
Sokoine, Mbeya.
Wapinzani wao katika mbio za
ubingwa wa Ligi Kuu, Azam
wameendelea kusuasua baada ya
kulazimishwa sare 1-1 na Ashanti
United, kama ilivyokuwa kwa
Coastal Union dhidi ya Rhino
Rangers 1-1. Vinara JKT Ruvu
wamepokea kipigo cha bao 1-0
kutoka kwa Ruvu Shooting na
kuondolewa kileleni na Simba.
Kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, mshambuliaji Tambwe
aliweka rekodi katika Ligi Kuu ya
Tanzania kwa kufunga mabao
manne katika mchezo mmoja.
Mrundi huyo aliwainua mashabiki
wa Simba katika dakika ya 4,
akiunganisha kwa kichwa krosi ya
Issa Rashidi, ambapo baadaye
winga Haruna Chanongo aliifungia
Simba bao la pili kwa shuti la
mguu wa kushoto akimalizia mpira
ulioshindwa kuokolewa vizuri na
mabeki wa Mgambo.
Tambwe aliipatia Simba bao la tatu
katika dakika ya 41, akimalizia
mpira uliomshinda kipa wa
Mgambo, Manzi. Mrundi huyo pia
alifunga bao la nne kwa Simba
katika dakika ya 44 akimalizia vizuri
krosi ya Amri Kiemba.
Naye Chanongo aliipatia Simba bao
la tano baada ya kuwazidi kasi
mabeki wa Mgambo katika dakika
ya 64. Kama hiyo haitoshi, Tambwe
alipachika bao la sita kwa Simba
kwa mkwaju wa penalti baada ya
Bashiru Chanache kushika mpira
kwenye eneo la hatari.
Kwenye Uwanja wa Chamazi,
mfungaji bora wa msimu uliopita,
Kipre Tchetche alifunga bao lake la
kwanza msimu huu wakati
alipoifungia Azam bao la kuongoza
katika dakika ya 21 akiunganisha
kwa shuti kali kona iliyopigwa na
Waziri Salum na kushindwa
kuokolewa vizuri na mabeki wa
Ashanti United.
Katika mechi hiyo, Azam walipata
pigo baada ya beki wao Aggrey
Morris kuonyeshwa kadi nyekundu
na mwamuzi Oden Mbaga baada ya
mchezaji huyo kumkwatua kwa
makusudi Hussen Sued wa Ashanti.
Katika dakika ya 79, Antony
Matanga’alu alisawazishia Ashanti
kwa mpira wa adhabu ndogo
uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Huko Mbeya, Utulivu mkubwa
ulitawala kwenye Uwanja wa
Sokoine, tofauti na ilivyokuwa
Jumamosi iliyopita dhidi ya Mbeya
City, wakati Prisons walipoikabili
Yanga mbele ya mashabiki
wachache. Prisons walianza kwa
kasi na kukosa bao dakika 2, baada
ya shuti la Ibrahimu Isaka kutoka
nje kidogo ya goli, Yanga walijibu
mapigo dakika ya 8, kupitia Didier
Kavumbagu.
Mshambuliaji Jerryson Tegete
aliifungia Yanga bao la kuongoza
katika dakika 42, akiunganisha krosi
ya Simon Msuva. Kabla ya Peter
Michael kuisawazishia Prisons
katika dakika ya 76 akimalizia krosi
ya Omega Seme.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑