JOHARI, CHUCHU HANS WAZICHAPA

image

Stori: Brighton Masalu
KIMENUKA! Waigizaji wenye
majina makubwa Bongo, Blandina
Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans
wanadaiwa kuchapana kisa
kikidaiwa kuwa ni penzi la
mwigizaji ‘kaka mkubwa’, Vincent
Kigosi ‘Ray’, Amani limenyetishiwa
mkanda kamili.
TUHUMA
Kwa mujibu wa chanzo cha habari
hizi makini ambacho ni rafiki wa
karibu wa wasanii hao, tukio hilo
lilijiri mwishoni mwa wiki
iliyopita ndani ya Ofisi za RJ
Productions, zinazomilikiwa kwa
ubia wa Ray na Johari zilizopo
Sinza-Mori jijini Dar ambapo
Johari alikuwa akimtuhumu
Chuchu mambo mazito ya
kimapenzi kwa Ray.
Shushushu huyo alitonya kuwa,
siku ya tukio Johari na wasanii
wenzake walikuwa wakirekodi
filamu ndani ya hoteli moja (jina
tunalo) iliyopo jirani na ofisi hizo
ndipo alipofikishiwa umbeya
kuwa Chuchu yuko kwenye ofisi
hizo ‘akijiachia’ na bosi mwenzake
(Ray), jambo lililotia ganzi moyoni
mwa mdada huyo.
MCHEZO MZIMA
‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai
kuwa baada ya Johari kupata
habari hizo, bila kujiuliza wala
kuvuta subira, ‘alisaga soli’ hadi
maeneo hayo.
“Alipofika aliingia ndani moja kwa
moja na kumvamia Chuchu huku
akimshushia kipigo chenye ujazo,”
kilidai chanzo hicho.
Alidai kuwa katika timbwili hilo,
Chuchu naye alifurukuta ndipo
wakazichapa laivu kabla ya Ray
aliyekuwa nje kusikia na kuwahi
kuokoa jahazi.
“Unajua kilichomshtua Ray ni kilio
cha Chuchu aliyekuwa akiomba
msaada baada ya kuzidiwa na
Johari,” kilidai.
Chanzo kilidai kuwa aliingia ndani
akiwa amefura na kufoka lakini
alikuwa ameshachelewa kwani
tayari Johari alikuwa
ameshaugeuza bucha mwili wa
Chuchu.
Ilidaiwa kuwa baadaye Ray
alimtoa nje Johari akimtaka kuwa
mbali na Chuchu.
SINEMA YA BURE
“Ilikuwa ni bonge la soo, watu
walijaa sana, baadaye Ray alimtoa
Johari nje huku akimfokea.
“Unaambiwa Johari alikuwa
akikimbia na Ray kumfukuza,
jambo lililovutia watazamaji wa
sinema hiyo ya bure,” alisema
mpashaji wetu.
JOHARI, CHUCHU WASAKWA
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo,
gazeti hili liliwasaka Johari na
Chuchu kwa nyakati tofauti.
JOHARI AKIRI
Kwa upande wake Johari alikiri
kutokea kwa kasheshe hiyo.
“Ni kweli lakini nani
amekuambia? Unajua
kilichoniudhi mimi ni maneno
machafu ya huyu dada (Chuchu)
anavyotamba kwa watu kuwa
amenipokonya mume, wakati
hakuna ukweli juu ya hilo,
nilishikwa na hasira sana ndiyo
maana nikaamua kumpa somo
kidogo.
“Inaniuma kwa sababu mimi na
Ray tumetoka mbali sana hadi
kuisimamisha RJ. Tulikuwa
hatuna kitu kabisa tukaungaunga
huku na kule hivyo Chuchu
anapaswa kutambua hilo. Asitake
kunikumbusha vitu vingi kwa
sababu tuliteseka sana,” alisema
Johari kwa uchungu.
VIPI BADO ANAKWENDA RJ?
“Tangu ile ishu itokee sijaenda RJ
kwa sababu Ray alinifukuza eti
kisa Chuchu. Usiniulize muafaka
wa hili jambo kwa sababu hadi
sasa sina majibu ya moja kwa
moja kuna vitu naviweka vizuri,”
alisema mwanadada huyo.
HUYU HAPA CHUCHU
Kwa upande wake Chuchu aliruka
kimanga kuwa hakuna ishu kama
hiyo.
“Aaah, jamani sina cha kusema
juu ya hilo, nikiwa tayari
nitawaambia.
“Kinachonishangaza kila Johari na
Ray wakigombana huwa natajwa
mimi. Yaani sijui hata haya
mambo yanatokea wapi,” alisema
Chuchu.
RAY
Gazeti hili lilipomtafuta Ray
kutaka kujua ukweli wa ishu hiyo,
bila kujibu ndiyo au hapana,
alimjia juu mwandishi:
“Sikia Brighton (mwandishi), hili
jina nimelitafuta kwa miaka
mingi. Nakuomba usiandike
habari hiyo, sielewi chochote.
“Ugomvi wao siujui na
wakigombana waache kunitaja,
waeleze sababu zao za
kugombana siyo kunitajataja
mimi,” alisema Ray na hata
alipoulizwa uhusiano wake na
wanawake hao aliishia
kujiumauma bila kutoa majibu ya
kueleweka.
HALI NI MBAYA
Habari za kina zilidai kuwa hali ni
mbaya kati ya mastaa hao ambapo
mashabiki wao waliozungumza na
gazeti waliiomba Kamati ya
Nidhamu ya Bongo Movie kuingilia
kati ugomvi huo ili kutafuta
ufumbuzi.
Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑