ICC yawaonya wanablogu nchini Kenya

image

Mahakama ya kimataifa ya ICC
imetoa onyo kali kwa wanablogu
nchini Kenya,wanaotoa taarifa
kuhusu mashahidi waliofika
mbele ya mahakama ya ICC. Hii ni
baada ya taarifa kuhusu shahidi
wa kwanza mbele ya mahakama
hiyo kujitokeza kwenye mitandao
hasa kwenye blogu, twitter na
Facebook kumhuusu.
Blogu hiyo ya udaku pia
ilichapisha picha ya mwanamke
huyo
Baadhi ya taarifa zilisema kuwa
amewahi kutoa ushahidi wake
ambao haukutofautiana na
alikiambia mahakama ya ICC,
katika mahakama nchini Kenya
lakini ukapuuziliwa mbali na
mahakama.
Mashahidi hao wanatoa ushahidi
wao ndani ya mahakama ila
wamefichwa nyuso zao hatua
iliyochukuliwa ili kuwalinda
kutokana na tisho lolote dhidi ya
maisha yao.
ICC huenda ikachukua hatua za
kisheria dhidi ya wanaosambaza
taarifa kuhusu mashahidi
wanaofika mbele ya mahakama
hiyo.
Jaji anayeongoza vikao hivyo, Chile
Eboe-Osuji, alisema kuwa ni
makosa kisheria kuwafichua
mashahidi wakati mahakama
imebana kuwatambulisha.
Shahidi huyo ambaye wenye blogu
wanasema wanamfahamu, ni
mwanamke mwathiriwa wa
shambulizi dhidi ya Kanisa la
Kiambaa ambako yeye na
wanakijiji wenzake walitafuta
hifadhi wakati wa ghasia za baada
ya uchaguzi kutokota katika mkoa
wa Rift Valley. Watu zaidi ya
thelathini waliteketezwa wakiwa
hai ndani ya kanisa hilo.
Chanzo – BBC Swahili

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑