Simba utamu, Yanga kwikwi

image

SIMBA jana ilijiongezea pointi
tatu katika safari ya kuwania
taji la Ligi Kuu Tanzania Bara
baada ya kuifunga Mtibwa
Sugar mabao 2-0 katika mechi
iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam.
Wakati Simba ikiutumia vizuri
uwanja wake wa nyumbani,
mtani wake Yanga alishindwa
tena kuendelea na kazi ya
ushindi aliyoanza nayo baada
ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi
ya Mbeya City katika mechi
iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Sokoine Mbeya.
Katika mechi ya Uwanja wa
Taifa, iliyokuwa ikisubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa soka,
Simba ilipata bao lake la
kuongoza katika dakika ya 67
kupitia kwa Henry Joseph.
Joseph aliyeingia kipindi cha
pili kuchukua nafasi ya Said
Khamis alifunga bao hilo baada
ya kuunganisha mpira wa kona
uliopigwa na Haruna
Chanongo.
Betram Mombeki aliifungia
Simba bao la pili katika dakika
ya 90 kufuatia kazi nzuri ya
Ramadhan Singano.
Katika mechi hiyo, timu
zilishambuliana kwa zamu,
kwani Mtibwa ilitawala mchezo
katika kipindi cha kwanza na
kusababisha wachezaji wa
Simba kupoteana ambapo
katika dakika ya 31, Amri
Kiemba aligongeana vema na
Amis Tambwe aliyempasia
mpira Chanongo lakini shuti
lake linapaa juu ya lango la
Mtibwa.
Lakini Simba iliibuka kipindi
cha pili na wachezaji wake
kucheza kwa kuonana zaidi na
ndiyo iliyochangia kupata
mabao hayo.
Aidha, Juma Lazio wa Mtibwa
Sugar alikosa nafasi ya wazi
katika dakika ya 8, lakini dakika
nane baadae Simba nao
walikosa bao baada ya Issa
Rashid ‘baba ubaya’ kupiga
vibaya mpira wa adhabu
ambapo ulidakwa na kipa wa
Mtibwa Hussein Sharif.
Katika dakika ya 55, Vicent
Barnabas alipata pasi ya
Masoud Mohamed lakini shuti
lake lilidakwa na kipa wa
Simba, Abel Dhaira.
Kutoka Mbeya, Yanga iliyoanza
ligi kwa ushindi wa mabao 5-0
dhidi ya Ashati United kabla ya
kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya
Coastal Union, jana ikatoka
sare kama hiyo jijini Mbeya.
Hali ya mchezo ilionekana kuwa
ngumu katika kipindi chote cha
kwanza na kusababisha timu
hizo kwenda mapumziko bila
kufungana japo viwango vya
kimchezo vilionesha hakuna
aliye mzoefu wala mgeni katika
michuano mikubwa kati ya timu
hizo mbili.
Dakika ya 49 ya mchezo, Mbeya
City wakawafanya mashabiki wa
Yanga kulowa baada ya
Mwagane Yeya kupachika bao
safi na la kiufundi alilolifunga
kwa kichwa.
Lakini dakika ya 70 ya mchezo
mashabiki wa Mbeya City
waliojitokeza kwa wingi
uwanjani hapo wakajikuta
wananywea baada ya Didier
Kavumbagu kupachika bao la
kusawazisha akitumia kifua
chake.
Hata hivyo, awali nusura
mchezo huo uingie dosari
baada ya watu wanaodaiwa
kuwa mashabiki wa Mbeya City
kulirushia makopo ya maji basi
lililobeba wachezaji wa Yanga
na kupasua kioo cha dirisha la
upande wa dereva na
kumjeruhi mkono wa kulia
dereva wa basi hilo, Maulid
Kiyula.
Nayo JKT Ruvu iliendelea kukaa
kileleni mwa msimamo wa ligi
hiyo baada ya kuifunga Ashanti
United bao 1-0 katika mechi
iliyochezwa kwenye uwanja wa
Azam Complex, Chamazi Dar es
Salaam.
Ushindi huo umeifanya JKT
Ruvu ifikishe pointi 9. Kutoka
Arusha, John Mhala anaripoti
kuwa wenyeji JKT Oljoro
walilazimishwa sare ya bao 1-1
na Rhino ya Tabora katika
mechi iliyochezwa kwenye
uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Rhino ilikuwa ya kwanza
kuandika bao la kuongoza
katika dakika ya tano ya mchezo
huo lililofungwa na Saad
Kipanga baada ya kujitangulizia
pasi ndefu kabla ya kuwatoka
mabeki wa Oljoro na
kuukwamisha mpira wavuni.
Dakika ya 26, Oljoro
wakasawazisha bao hilo kupitia
kwa Amir Omati baada ya
kutokea piga nikupige langoni
mwa Rhino.
Kwenye Uwanja wa Kaitaba
Bukoba, Kagara Sugar
ililazimishwa sare ya bao 1-1
na Azam, huku Coastal Union
nayo ikishindwa kuutumia
vizuri uwanja wa Mkwakwani
Tanga baada ya kutoka suluhu
na Prisons ya Mbeya.
Aidha kwenye uwanja wa
Mabatini Mlandizi, Ruvu
Shooting iliibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑