Mzungu afanya wizi wa kutisha bandari Dar

image

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe amebaini
kuwepo kwa wizi mkubwa wa
mafuta aina ya petroli katika
bandari ya Dar es Salaam
unaofanywa na mzungu
anayetajwa kuiba kiasi cha lita
20,000 kila siku baada ya
kutoboa boya kubwa la
kupakulia mafuta (SBM).
Ingawa haukutajwa uraia wa
mzungu huyo, imeelezwa baada
ya kuiba kiasi hicho kikubwa
cha petroli akiwatumia walinzi
wa kitanzania, hujaza kwenye
maputo.
Hayo yalibainika jana wakati
Waziri Mwakyembe alipofanya
ziara na kuzungumza na
wafanyakazi wa Mamlaka ya
Bandari (TPA) na Wakala wa
Ndege za Serikali.
Akiwa bandarini, Dk
Mwakyembe aliahidi
kupambana na mzungu huyo
anayetumia walinzi wa
kitanzania wa kampuni
inayolinda boya hilo ambayo
hakuwa tayari kuitaja kwa jina
kwa kuhujumu nchi na kusema
ataondoa ‘uzungu wake’
unaompa kiburi cha kufanya
wizi.
Haikuelezwa amefanya wizi
huyo kwa muda gani. Alisema
kwa kushirikiana na Wizara ya
Nishati na Madini wanafanya
kazi hiyo kutafuta aliyewatuma
watu hao akiwemo mzungu
huyo ili kuweza kumchukulia
hatua za kisheria.
“Nitapambana na huyo mzungu
kwa nguvu zangu zote na
kuondoa uzungu wake ili
kumfikisha katika vyombo vya
sheria,” alisema huku
akionesha picha ya boya hilo
lilivyotobolewa.
Aliwaagiza askari wa bandari
kuhakikisha ifikapo kesho
(Jumatatu) saa 6:00 mchana
majina ya askari wa kampuni ya
ulinzi wanaolinda boya hilo
waliotumika kuiba yanakuwa
kwake.
Alisema inaonekana askari hao
wa kampuni inayolinda
wanahusika kutokana na wiki
iliyopita ilipobainika wizi huo
walikurupushwa wabadhirifu
hao na kukimbia kisha
kuangusha bunduki.
“Ni dhahiri wanaofanya wizi
huu ni wataalamu, kwani
wanafungua na kufunga
kitaalamu, jambo ambalo mvuvi
wa kawaida hawezi kutokana na
kuhitaji kukaa chini ya maji kwa
saa sita,“ alisema.
Mwakyembe alisisitiza kuwa
baada ya kubainika kwa askari
waliohusika watafunguliwa kesi
ya kuhujumu uchumi, kwani
boya hilo lilijengwa kwa mkopo
wa dola za Marekani milioni 60
(Sh bilioni 97.8) ambazo ni
mkopo na bado serikali
haijaanza kuulipa.
Pia aliitaka Kampuni ya
Kimataifa ya Kuhifadhi Mafuta
(TIPER) kama wanataka suluhu
na serikali kuvunja mkataba na
kampuni hiyo ya ulinzi
inayotuhumiwa kwa wizi huo
kuanzia kesho.
“Ninachotaka ni kumfahamu
aliyewatuma na kumchukulia
hatua huku kampuni ile ya
ulinzi Jumatatu (kesho) ilete
picha zote za walinzi waliokuwa
zamu siku ile ili tulipie kwa
kutoa magazetini kwa nia ya
kuwatafuta,” alisema.
Alisisitiza kuwa, pia atahitaji
picha za walinzi wote
waliokuwa wakilinda boya ili
baada ya upelelezi kukamilika
wawekwe hadharani. Aidha,
Mwakyembe aliwapongeza
wafanyakazi wa bandarini kwa
kazi nzuri wanayofanya sasa,
licha ya kuwepo kwa
changamoto kadhaa na
kubainisha kuwa utatuzi
umebaki katika bodi, kwani
kuna mpasuko.
Alisema haiwezekani kuendelea
kuangalia yeye ana ‘saruji’ kali
ya kuziba mpasuko huo na
atafanya hivyo kabla ya kesho
kwani ni sababu ya kuzorotesha
utendaji kazi wa bandari.
“Udokozi sasa umepungua hadi
baadhi ya nchi kama Zimbabwe
wamepongeza, sasa mpasuko
huu wa bodi nitaumaliza
mapema na kuanzia sasa katika
bodi hiyo kutakuwa na mjumbe
mmoja ambaye ni mwakilishi
wa wafanyakazi ili
kuwawakilisha,” alisema.
Waziri huyo pia alisema
kuanzia sasa ni marufuku
kupeleka boti au meli
kutengenezwa Mombasa nchini
Kenya na ikishindikana
kufanyiwa matengenezo
bandari ya Dar es Salaam, basi
waombe kibali kwake au kwa
katibu mkuu wa wizara ya
uchukuzi ili kusaidia katika
kuomba jeshi kutengeneza,
kwani ni aibu kuendelea
kupeleka Mombasa.
Pia aliagiza muundo wa ajira
kwa wafanyakazi wa bandari
uwe umekamilika kufikia
mwisho wa mwaka huu na
kuhakikisha vibarua waliokaa
muda mrefu wanaajiriwa katika
nafasi walizopo na siyo
kupelekwa waajiriwa wapya.
Akizungumza katika kikao hicho,
Kaimu Mkurugenzi wa TPA,
Madeni Kipande alisema
kutokana na maelekezo ya
Waziri Mwakyembe aliyoyatoa
Desemba mwaka jana
wameweza kuongeza posho kwa
wafanyakazi za usafiri kuwa Sh
200,000 na chakula Sh 100,000
pamoja na kuongeza malipo ya
kufanya kazi muda wa ziada.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑