JK aahidi kuezeka nyumba ya Cheka

image

RAIS Jakaya Kikwete
amemtumia salamu za pongezi
bondia wa ngumi za kulipwa
nchini, Francis Cheka (SMG) na
pia ameahidi kutoa mchango
wake binafsi kuezeka bati
nyumba ya bondia huyo
atakapokamilisha ujenzi wake
baada ya kupatiwa kiwanja cha
makazi na serikali ya mkoa wa
Morogoro.
Pongezi za Rais Kikwete na
ahadi yake zilitolewa na Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel
Bendera, wakati akiwahutubia
mamia ya wananchi wa
Manispaa ya Morogoro
walioshiriki kwenye tafrija ya
kumpongeza bondia huyo
kwenye Uwanja wa Shujaa, Kata
ya Mji Mpya, mjini hapa juzi.
Katika tafrija hiyo ya aina yake
kufanyika mkoani hapa,
wananchi walijipanga mistari
kujipatia chakula na vinywaji
na kutokana na chakula kuwa
kingi, watu waliruhusiwa
kupeleka nyumbani.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa,
Rais Kikwete ameungana na
wananchi wa Morogoro
kumpongeza Cheka na pia
amemwambia kuwa ataezeka
nyumba hiyo baada ya
kujengwa ukiwa ni mchango
wake binafsi akitambua
mchango wa Cheka kitaifa na
kimataifa.
“Mheshimiwa Rais Kikwete
aliposikia mkoa umetoa kiwanja
cha makazi kwa bondia Cheka,
yeye binafsi amenitumia
salamu niwajulishe kuwa yupo
pamoja nasi kwa kumpongeza,”
alisema.
“Amenipa ahadi yake kwa
kusema baada ya kukamilika
kujengwa kwa nyumba hiyo
gharama za kuiezeka zitakuwa
ni zake binafsi …hivyo sisi
wananchi wa Morogoro hatuna
budi kumshukuru Rais kwa
kitendo chake ya kutuunga
mkono,” alisema Bendera
mbele ya umati wa wananchi
uwanjani hapo.
Serikali ya mkoa wa Morogoro
chini ya mkuu wa mkoa huo,
iliandaa tafrija ya wazi kwenye
uwanja huo na kujumuisha
viongozi wa serikali, siasa, dini,
wanamichezo pamoja na
wananchi wanaoishi Manispaa
ya Morogoro.
Pia tafrija hiyo ilitumiwa na
wadau mbalimbali,
wafanyabiashara na viongozi wa
serikali kumkabidhi bondia
huyo zawadi, ambapo Manispaa
ya Morogoro ilitoa ‘ofa’ ya
kiwanja cha makazi na
kumpatia Mkuu wa Mkoa
ambaye alimkabidhi Cheka.
Zawadi nyingine zilizoahidiwa
kwa bondia huyo ni tani nne za
saruji kutoka Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa, wakati Ofisi ya CCM
Wilaya ya Morogoro mjini
kichama, kikibeba jukumu la
kuchora michoro ya ramani ya
kiwanja cha nyumba hiyo.
Mbali na hayo, Mkuu wa Wilaya
ya Mvomero, Anthony Mtaka,
ambaye pia ni Rais wa
Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT), alisema kuwa wilaya hiyo
imemzawadia bondia huyo
kiwanja kimoja eneo la
Mvomero.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro
mjini, Abdulaziz Abood, kwa
upande wake ametoa tofali
1,000 na Mkurugenzi wa
Kampuni ya ATN Petroleum Ltd,
Abdullatif Talib, ameahidi
kumpatia sh milioni tano,
wakati wadau wengine wawili
wametoa Sh milioni 1.5.
Bendera alisema, mafanikio ya
Cheka yamechangiwa na
walimu wake wa ngumi na kwa
kutambua mchango huo, mkoa
utampatia kocha wake, Abdul
Salehe ‘ Komando’ Sh milioni
moja.
Bondia Cheka amejipatia
umaarufu mkubwa ndani na
nje ya nchi baada ya
kumtwanga kwa pointi bondia
Phill Williams kutoka Marekani,
Agosti 30, mwaka huu kwenye
pambano la uzani wa kati na
kunyakua mkanda wa ubingwa
wa dunia wa Shirikisho la
Ngumi wa Duniani (WBF).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑