Bunda wahofia uhai wa Chadema

image

wanachama na viongozi wa kata
nne wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA)
Jimbo la Bunda, mkoani Mara
wameelezea kuhofia uhai wa
chama hicho jimboni humo na
kutaka uongozi wa juu
kuchukua tahadhari, kwa madai
kuwa wapo wanaoteka chama
kwa maslahi yao binafsi.
Katika tamko lao jana baada ya
kikao kilichodumu kwa saa nne
kilichojumuisha viongozi na
baadhi ya wanachama wa kata
nne za mjini Bunda, walidai
chama kinaongozwa na mtu
mmoja kinyume cha Katiba ya
chama hicho.
Walimshutumu Mwenyekiti wa
chama hicho Taifa Freeman
Mbowe, wakidai kuwa
alishinikiza kuvunjwa kwa
uongozi wa kikatiba na kuteua
mtu mmoja kusimamia chama
hicho kama mali binafsi.
“Lengo la tamko hili ni kutaka
wanachama na wapenzi wa
CHADEMA kuelewa kuwa hivi
sasa chama hiki jimbo la Bunda
kinamilikiwa na mtu mmoja tu
Samwel Imanani aliyepatikana
kinyume cha katiba na
anatumia jina la chama kwa
shughuli zake binafsi,” alisema
Mwenyekiti wa kikao hicho,
Zablon Makoye.
Pamoja na mambo mengine,
walidai kiongozi huyo hutumia
vibaya jina la Chadema ambapo
amehamasisha mashindano ya
mpira wa miguu unaoendelea
ndani ya jimbo hilo kupitia
kada anayedaiwa kutaka
kuwania ubunge jimboni humo
mwaka 2015, Pius Masululi.
Katika tamko lao walitaka
mfadhili wa mashindano hayo
kutoita mashindano hayo kwa
jina lake la ‘PIUS CUP’ badala
yake atumie ‘CHADEMA CUP’
kwa madai kuwa ametumia
chama kuandaa mashindano
hayo hivyo afute jina lake.
Aidha walimtaka kuja binafsi
jimboni humo kama wengine
wanaofadhili michezo
wanavyofanya bila kupitia
vyama vya siasa na angeonesha
nia yake muda ukifika.
Tamko hilo lilidai kada huyo
huzunguka katika kata za jimbo
hilo kwa kugawa bendera za
chama, mipira na kuhamasisha
jamii kumuunga mkono bila
vikao husika vya chama.
Hata hivyo, kiongozi huyo
anayesimama pekee jimboni
humo kama kiongozi wa
CHADEMA, Samwel Imanani
amekiri uongozi wa juu wa
CHADEMA kumteua kusimamia
shughuli zote za chama
jimboni humo hadi uchaguzi
wa kikatiba utakapofika.
Imanani alisema kuwa taratibu
zote za mashindano
yaliyodhaminiwa na kada wa
CHADEMA, Pius Masululi
yamekidhi masharti na kwamba
madai ya wanachama hao
hayana msingi bali ni chuki
binafsi.
Kwa upande wake Masululi
amewaeleza waandishi wa
habari kuwa kamwe
mashindano hayawezi kuitwa
kwa jina la chama cha siasa
kwani hiyo itamaanisha
ubaguzi wa kiitikadi.
“Ni kweli mimi ni kada wa
CHADEMA na nimeanzisha
mashindano haya ili kukuza
vipaji vya vijana wanaopenda
soka ndani ya jimbo la Bunda,
lakini pia kuikienzi CHADEMA,”
alisema Pius na kuongezea.
“Mimi kama mfadhili wa
mashindano siwezi kuita
mashindano kwa jina la chama
changu, watu wakisikia
mashindano yanaitwa
CHADEMA CUP ambao hawana
itikadi ya CHADEMA
hawatashirki nitakuwa
nimefanya ubaguzi wa ajabu,
hayo madai hayalengi umoja.
“Kama leo kada wa CHADEMA
ameita mashindano kwa jina la
CHADEMA CUP, kesho kada wa
CCM ataita CCM CUP, CUF nayo
itaita, TLP nayo……huu ni
ubaguzi” alisema .
Alieleza kuwa mashindano hayo
hivi sasa yanaendelea katika
kata zote za jimbo la Bunda
kwa lengo la kuinua vipaji vya
vijana wanaokosa fursa ya
michezo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑