MZEE MAJUTO AKIMBIA NDOA

image

MWANAMKE anayedaiwa kufunga
ndoa ya siri na mchekeshaji mahiri
Bongo, Amri Athuman maarufu
kama Mzee Majuto au King Majuto,
Rahma Abdallah (20), ameibuka na
kudai kutelekezwa na mumewe
huyo.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwa siri
jijini Dar Julai 28, mwaka huu na
kudumu siku 44, inaonekana
imevunjika rasmi baada ya Mzee
Majuto kutoa talaka kupitia kwa
msanii wa filamu aitwaye Rehema
Omary.
WOTE NI WAJA LEO, WANDOKA LEO
Akizungumza na gazeti hili katika
ofisi zetu, Bamaga-Mwenge, Dar,
Septemba 9, mwaka huu, Rahma
alidai kuwa alikutana na Mzee
Majuto jijini Tanga na kuanzisha
uhusiano wa kimapenzi kwa miezi
sita kabla ya kufunga ndoa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani uliopita.
“Tulifahamiana Tanga, mimi ni
mwenyeji wa huko kama ilivyo kwa
Mzee Majuto, wakati tukiwa kwenye
uhusiano, ulipofika Mwezi wa
Ramadhani akaona bora tufunge
ndoa ili tusiendelee kutenda
dhambi, akaniambia dhamira yake
hiyo nami sikukataa,” alisema
Rahma.
TOFAUTI MIAKA 40
Mke huyo ambaye ni kibinti cha umri
wa miaka 20 aliyepishana na Mzee
Majuto kwa umri wa miaka 40
alisema kuwa, mwigizaji huyo
alifuata taratibu zote za kufunga
ndoa kwa kupeleka barua ya posa
nyumbani kwao.
“Alitoa mahari ndipo ilipopangwa
siku ya ndoa iliyofungwa nyumbani
kwa mama yangu, Mbagala-Zakhem,
Dar,” alifafanua Rahma.
ULINZI MKALI, BARAFU MPAMBE
Katika ndoa hiyo iliyofungwa katika
Mtaa wa Kibonde-Maji Julai 28,
mwaka huu na Shehe Abdurahman
Kisoma na kufuatiwa na sherehe
nyumbani kwa bibi harusi, ulinzi
mkali uliwekwa ili siri ya Mzee
Majuto kuoa isivuje.
Mashahidi wa ndoa hiyo walikuwa ni
Suleiman Said ‘Barafu’ ambaye ni
mwigizaji aliyekuwa mpambe wa
bwana harusi pamoja na Mohammed
Malila.
MAHARI 20,000
Cheti cha ndoa hiyo, kinaonesha
kwamba Mzee Majuto alimuoa
mwanamke huyo kwa mahari ya
shilingi 20,000 aliyolipa yote.
“Baada ya ndoa, Mzee Majuto
aliwaomba wazazi wangu nikae
nyumbani hadi Mwezi wa Ramadhani
utakapoisha ndipo atakapokuja
kunichukua, akaniachia shilingi elfu
sitini tu, mpaka leo hii sijamuona,”
alisikitika mke huyo ambaye alikuwa
akijua kama Mzee Majuto alikuwa na
mke mwingine.
KAZI KWA PROFESSA J
Mke huyo wa Mzee Majuto alisema
kuwa kabla ya kufunga ndoa na gwiji
huyo wa uchekeshaji alikuwa
akifanya kazi katika saluni ya
mwanamuziki Joseph Haule ‘Profesa
Jay’ iliyopo Msasani, Dar.
“Nilikuwa nafanya kazi na kupata
kipato huku nikiwa nimepanga
chumba lakini Majuto aliniambia
niache kazi na nirudishe chumba,
nami nikafanya hivyo nikijua naenda
kuishi kwa mume wangu, kumbe!…”
alijuta Rahma.
MESEJI CHAFU ZA MKE MKUBWA
Baada ya Majuto kuondoka mke huyo
alikuwa akimpigia simu kutaka fedha
za matumizi lakini alikuwa akiambiwa
awasiliane na Bi. Rehema,
mwanamke ambaye Mzee Majuto
huwa anaigiza naye katika filamu
zake.
Rahma alilalamika kutumiwa ujumbe
wa matusi kwenye simu yake na mke
mkubwa wa Mzee Majuto.
“Kitendo hicho kinaniuma sana kwani
wakati mwingine huwa ananitukana
na kunitishia maisha, akidai eti
atanifanyia kitu kibaya, nikimpigia
Majuto na kumweleza naye ananijibu
mbovu,” aliongeza.
Mke huyo mdogo wa Mzee Majuto
alisema kuwa anaumia kutokana na
kuharibiwa maisha kwa kuolewa na
kuachishwa kazi huku akiendelea
kutukanwa na mke mkubwa.
MASHITAKA BAKWATA
Rahma ambaye aliliachia Amani
nakala ya cheti cha ndoa alisema
msanii huyo amemdhalilisha kwani
kila akidai talaka yake anamwambia
ameshaituma kwa Bi. Rehema na
kumtaka aende akaichukue kitu
ambacho ni kinyume na makubaliano
yao.
Rahma alisema kuwa amejipanga
kwenda kumshitaki Mzee Majuto
katika Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (Bakwata) ili amlipe fidia
na kumtafutia kazi.
“Yeye ndiye aliyenioa lakini nikimdai
talaka ananimbia alimpa Bi.Rehema,
wakati mwanamke huyo siye
aliyenioa, sasa nampeleka Bakwata
ili anikabidhi talaka na kunilipa
fidia,” alisema kwa hasira mke huyo.
MSIKIE MZEE MAJUTO
Akijibu tuhuma hizo akiwa jijini
Tanga, Mzee Majuto alikiri kufunga
ndoa na Rahma na kusema kuwa
alishamuacha kwa sababu aligundua
hajatulia.
“Huyo mwanamke nimeshaachana
naye ila kwa sasa anataka
kunichafua, kama anahisi ana haki
kwa nini asiende mahakamani?
Nimemtuma mshenga ampe talaka
hataki kuipokea, anataka nije Dar.
Kama huo siyo uhuni ni nini? huyo
mwanamke hajatulia,” alisema.
TALAKA KULETWA GLOBAL
Mzee Majuto alidai kwamba, Rahma
amekuwa akimpa usumbufu na
kufikia kumpa masharti ya ajabu na
kuahidi kumtuma mtu ailete nakala
ya talaka hiyo katika ofisi za gazeti
hili (Global).
source. globalpublishers.info

posted by kulwa ngatigwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑