NYUMBA YA ASHA BARAKA YATEMBEZEWA NYUNDOZZZ ENEO LA HANANASIFU JIJINI DAR

image

Mkurugenzi wa bendi ya African
Stars ‘Twanga Pepeta’, ambaye
pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha
Baraka, akiwaka wakati
akizungumza  na mtandao huu
jana jioni alipokuwa akisimamia
zoezi la kuwazuia wabomoaji
kutobomoa nyumba na vibanda
vya wananchi katika eneo hilo la
Hanansifu bila kufikia muafaka
kwa mazungumzo na wahusika.
Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo
ili kujengwa barabara ya mtaa
lilianza tangu mwezi wa tano
mwaka huu, ambapo wenye
nyumba zizizopo eneo hilo baada
ya mazungumzo na wasimamizi
wa zoezi hilo na Diwani na
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
huo, walikubaliana na kuwekewa
alama eneo linalotakiwa
kubomolewa ili kupisha upanuzi
huo.
Baada ya alama hizo ulifanyika
ubomoaji na kuchimba barabara
hiyo kana kwamba zoezi la
ujenzi lilikuwa likianza muda
mfupi tu baada ya ubomoaji,
lakini cha kushangaza watu wao
baada ya kubomoa waliondoka
zao na kuacha eneo hilo likiwa
na madimbwi makubwa yaliyojaa
maji na kusababisha eneo hilo
kutopitika kwa wenye magari na
waenda kwa miguu.
Aidha baada ya kumalizika kwa
ubomoaji huo, wahusika wenye
nyumba zao na fremu za maduka
eneo hilo, walikaa kwa muda wa
miezi miwili na
walipohakikishiwa kuwa zoezi
hilo limemalizika na hakuna
ubomoaji utakaoongezeka,
walianza kukarabati nyumba na
fremu zao upya ili kuendelea na
biashara.
Cha kushangaza ghfla watu hao
walirejea tena jana na kuchora
alama mpya kwa kutumia mkaa,
na kuanza kubomoa jana hiyo
hiyo jambo lililowaacha hoi
wananchi wa eneo hilo na wenye
frem zao, kutokana na
kutotolewa kwa taarifa wala
watu hao kutokuwa na kiongozi
hata mmoja wa Eneo hilo yaani
Diwani au Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa, ambao
walitakiwa kuwepo ili kutoa
ufafanuzi wa tukio hilo.
Lakini cha kushangaza wakati
wa zoezi hilo, hakuwepo
Mwenyekiti wala Diwani, jambo
lililowafanya wananchi kuhoji
juu ya uhalali wa zoezi hilo.
Wakati wa zoezi hilo Asha
Baraka, alimpigia simu Diwani,
Abasi Tarimba, lakini naye
alimjibu kuwa hajui lolote kama
Diwani na kumtumia namba ya
simu ya mtu mwingine ili
azungumze naye, wakati yeye
ndiye hasa alitakiwa kuwapo
eneo hilo na kuwatetea wapiga
kura wake.
Hata hivyo watu waliokuwapo
eneo hilo walishangazwa na
kitendo cha jamaa hao kuendelea
kumoboa upande mmoja wa eneo
hilo huku wakikwepa ukuta wa
ghorofa lililopo eneo hilo ambalo
ni jipya lililojengwa hivi
karibuni kwa kukwepa gharama,
wakati alama za awali
zinaonyesha kuwa hata ukuta
wa ghorofa hilo ulitakiwa
kubomolewa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑