KITALE : MWANANGU ANAKOPI UTEJA by GLOBAL

image

MTU wangu mambo vipi?
Naamini uko poa na
unaendeleza harakati za
kusogeza maisha kama kawaida.
Kupitia kona hii ya Staa na
Mwana kama ilivyo ada,
tunayamulika maisha ya staa
mwenye mtoto ili kujua anaishi
vipi nyumbani kwake.
Wiki hii tunaye mchekeshaji
maarufu Bongo, Musa Yusuph
‘Kitale’ ambaye anaishi
Mwananyamala jijini Dar ,
Kwa upande wake amejaliwa
kupata mtoto mmoja kwa
mkewe, Fatuma Salum . Mtoto
wao wamempa jina la Hemedi.
Kumjua zaidi , ungana nami
katika mahojiano niliyofanya
naye:
Staa na Mwana : Mambo vipi
Kitale?
Kitale: Salama kabisa, karibu
sana nyumbani.
Staa na Mwana : Wewe ni mtu
wa masihara sana mbona
kwenye ulezi haufanyi tabia
hiyo?
Kitale: Unajua tena sanaa nje
tu, ukifika ndani lazima uwe
mpole, huwezi kuleta usanii
kwenye malezi ya mtoto ndiyo
maana unaniona niko makini
katika kumwandalia mwanangu
msosi wa nguvu.
Staa na Mwana : Je, ikitokea una
kazi ya sinema muda ambao
mwanao anataka chakula,
inakuwaje?
Kitale: Naanza kumhudumia
mwanangu kwanza na sinema
itakuja baadaye.
Staa na Mwana : Unataka
kuniambia hata kama ni mama
yake anataka haki ya ndoa
itabidi asubiri kwanza ?
Kitale: ( Kicheko) ndiyo anasubiri
kwanza , yeye atasikilizwa
baadaye.
Staa na Mwana : Unajisikiaje
kuitwa baba Hemedi?
Kitale: Jina hilo linafanya
nitembee kifua mbele , furaha
niliyo nayo juu ya mtoto wangu
haina mfano.
Staa na Mwana : Kuna tofauti
yoyote kabla hujapata mtoto na
ulipompata?
Kitale: Tofauti ni kubwa , zamani
unaweza ukajijali wewe
mwenyewe lakini sasa hivi
lazima mtoto wangu awe wa
kwanza kwa kila kitu.
Staa na Mwana : Vipi anaijua
kazi unayoifanya ?
Kitale: ( Akamuita) hebu
muonyeshe anti (mwandishi )
zile za Kitale ni zipi? Anazijua,
anakopi na kupesti.
“Oyaaa! Mwanangu
usinizingueee!” alisikika mtoto
huyo.
Staa na Mwana : Kumbe anajua
baba yake anavyofanya, huogopi
kama inaweza kuwa tatizo
kwake kwa kujiingiza kwenye
uvutaji wa madawa kweli?
Kitale: Siyo rahisi kwa sababu
huwa ninamueleza kila siku
kuwa ninapoigiza uteja nafanya
kama kazi ya sanaa hivyo
kamwe asithubutu kutumia
kwani yana madhara .
Staa na Mwana : Nini ambacho
hupendi kitokee kwa mwanao ?
Kitale: Sipendi mtu ampige
mwanangu maana akilia huwa
nahisi kuchanganyikiwa .
Staa na Mwana : Unapenda
akiwa mkubwa afuate nyayo
zako?
Kitale: Mimi napenda akiwa
mkubwa asome kwanza halafu
mwenyewe atachagua kazi ya
kufanya.
Staa na Mwana : Kitale
nikushukuru sana.
Kitale: Karibu tena na tena

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑