BUNGE LACHAFUKA

image

-WABUNGE CHADEMA , CUF ,
NCCR WATOKA NJE
WAKIPIGANIA ZANZIBAR
MUSWADA wa marekebisho ya
pili ya Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83 umezua
balaa bungeni , baada ya
wabunge wa Kambi ya
Upinzani , bila kujali itikadi za
vyama kutoka nje ya Bunge .
Wabunge waliotoka nje ya
Bunge ni wa vyama vya
Chadema, CUF na NCCR-
Mageuzi, ambao walikuwa
wakishinikiza Muswada huo
usisomwe hadi maoni ya wadau
kutoka Zanzibar yapatikane .
Hata hivyo, katika hali ya
kushangaza kwa siku ya jana,
Mbunge wa Konde , Khatibu
Said Haji (CUF) , aliwaongoza
wenzake kutoka Chadema,
NCCR-Mageuzi na CUF kutoka
nje, huku Mbunge wa Vunjo,
Augustine Mrema (TLP ), yeye
akibaki ndani ya Bunge .
Dalili za wabunge hao kutoka
nje ya Bunge , kama njia ya
kuwasilisha hisia zao kwa
Watanzania zilianza kuonekana ,
baada ya Msemaji wa Kambi
Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya
Sheria na Katiba , Tundu Lissu ,
kusema ili kutimiza matakwa ya
Sheria na kwa kuzingatia
mapendekezo ya Rasimu ya
Katiba iliyotolewa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Bunge
linahitaji kuangalia upya suala
la uwakilishi wa Zanzibar katika
Bunge Maalum .
Alisema kwa mujibu wa kifungu
cha 22( 2) cha Sheria, idadi ya
wajumbe wa Zanzibar katika
Bunge Maalum watatokana na
makundi yaliyoainishwa katika
kifungu cha 22 (1 )( c) .
Alisema hali hiyo, ina maana
kwamba uchache wa wajumbe
Zanzibar, hawatapungua 55
ambapo Rasimu ya Katiba
itakayojadiliwa na Bunge
Maalum inahusu Katiba ya
Jamhuri ya Muungano peke
yake.
Rasimu hiyo, imependekeza
masuala yote yasiyo ya
Muungano ya Washirika wa
Muungano, yaani Tanzania Bara
na Zanzibar , yashughulikiwe na
Katiba za Washirika hao.
Lissu, alisema kwa sasa
wabunge wanaotoka Zanzibar
katika Bunge la Muungano ni
83, wakati Baraza la Wawakilishi
Zanzibar lina wajumbe 76.
“Kwa ujumla, ili kutekeleza
matakwa ya kifungu cha 22 (1 )
na ( 2) cha Sheria, Zanzibar
itakuwa na wajumbe 219 katika
Bunge Maalum lenye wajumbe
604 , sawa na takriban asilimia
36 ya wajumbe wote .
“Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, inataka kujua kama
ilikuwa busara na sahihi kwa
nusu ya wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kutoka
Zanzibar, kwa nini isiwe busara
na sahihi vile vile kwa nusu ya
wajumbe wa Bunge Maalum
litakaloijadili na kuipitisha
Katiba Mpya hiyo kutoka
Zanzibar?
“Au ndio kusema hoja za usawa
kati ya nchi Washirika wa
Muungano huu ni kelele za
majukwaani tu ? Kwa sababu
hiyo, na kwa kuzingatia
mapendekezo ya ‘hadhi na haki
sawa’ baina ya Washirika wa
Muungano yaliyoko katika
Rasimu ya Katiba,” alisema
Lissu.
Alisema hali hiyo inawezekana
kwa kuongeza idadi ya wajumbe
waliotajwa katika kifungu cha
22(1 )( c) hadi 354 , kama
ilivyopendekezwa katika maoni
ya Kambi ya Upinzani .
Alisema kwa kurekebisha
kifungu cha 22 (2 ) ambacho
kitasomeka kwamba, idadi ya
wajumbe kutoka Zanzibar
haitapungua asilimia 55 ya
wajumbe hao kama pendekezo
hilo litakubaliwa na Bunge.
Alisema wajumbe wa Bunge
Maalum kutoka Zanzibar ,
wataongezeka kutoka 214 kwa
mujibu wa Sheria ilivyo sasa,
hadi 323 .
Rais apingwa
Katika maoni ya Kambi Rasmi ya
Upinzani , imepinga vikali
mapendekezo ya kumwezesha
Rais kuteua Wajumbe wa Bunge
Maalum wasiotokana na Bunge
lako tukufu na Baraza la
Wawakilishi Zanzibar .
“Wajumbe wanaopendekezwa
kuteuliwa kwenye Bunge la
Katiba kwa mujibu wa ibara ya
20(2 )( e) na (4 ) ya Muswada
Mpya sio , na hawawezi kuwa,
wawakilishi wa wananchi.
“Kwanza, hawajachaguliwa na
mtu yeyote na wala taasisi zao
kuwawakilisha katika Bunge la
Katiba kwa sababu Muswada
Mpya unapendekeza wateuliwe
na Rais .
“Kwa sababu ya upinzani huo,
mapendekezo ya kumfanya Rais
kuwa mteuzi wa wajumbe wa
Bunge Maalum wasiokuwa
wabunge na Wawakilishi
yaliondolewa katika Muswada
huo wa Sheria hii.
“Badala yake , kifungu cha 22 (1 )
(c ) cha Sheria iliyotungwa na
Bunge lako tukufu kiliweka wazi
kwamba “ wajumbe mia moja
sitini na sita watateuliwa
kutoka kwenye taasisi
zilizotajwa, ” alisema Lissu .
Hata hivyo Kambi hiyo ya
Upinzani iliingiwa na hofu na
Serikali ya CCM kudhibiti
muswada huo kutokana na
wingi wabunge kutoka chama
tawala.
CHANZO: MTANZANIA
SEPTEMBA 05, 2013

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑