RWANDA SASA YACHEZA RAFU

image

RWANDA imeamua ‘ kucheza
rafu’ kwa kuanza kuhujumu
Bandari ya Dar es Salaam , kwa
kupandisha ushuru wa
barabara kwa magari ya mizigo
yanayotoka Tanzania pekee
kuanzia Rusumo hadi Kigali,
kutoka dola za Marekani 152 za
awali, hadi 500 .
Kwa mujibu wa taarifa za
uhakika kutoka ndani ya kikao
cha Baraza la Mawaziri wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki
kilichomalizika hivi karibuni
Arusha, ushuru huo ulianza
kutozwa rasmi kwa magari hayo
juzi.
Hali hiyo imesababisha
mtafaruku katika eneo la
Rusumo, mpakani mwa
Tanzania na Rwanda, ambako
zaidi ya malori 200 yenye
mizigo kutoka Bandari ya Dar es
Salaam , yamekwama kwa
kushindwa kulipa kiwango hicho
kipya cha ushuru wa barabara .
Awali nchi hiyo ilikuwa ikitoza
ushuru wa dola za Marekani 16
kwa kila kilometa 100 , ushuru
ambao ndio uliokuwa ukitozwa
na Tanzania kwa malori
yaliyokuwa yakipitisha mizigo
kwenda nchi za nje .
Hata hivyo, katika
kilichoonekana kuwa mazingira
yasiyo sawa ya kupata faida
kutokana na udogo wa eneo wa
nchi hiyo , Rwanda iliamua
kupandisha ushuru huo, kutoka
dola 16 kwa kilometa 100 , hadi
dola 152 bila kuzingatia
kilometa.
Kabla ya kupandishwa kwa
ushuru huo, Tanzania
ilionekana kupata faida , kwa
kuwa kutoka Dar es Salaam
hadi Rusumo , ni kilometa 1 ,350
na hivyo kwa ushuru wa dola 16
kwa kilometa 100 , Serikali
ilipata dola 216 kwa gari.
Kwa Rwanda taarifa zinaeleza
kuwa hali ilikuwa tofauti
kutokana na udogo wa nchi ,
ambapo kutoka Rusumo hadi
Kigali ni kilometa 139 , ambao
kwa ushuru huo wa dola 16 kwa
kilometa 100 , Serikali ya
Rwanda ilijikuta ikiambulia dola
22.24 tu kwa gari.
Kutokana na mazingira
yaliyoonekana ya kutopata sawa
na Tanzania , yaliyotokana na
udogo wa nchi husika , Rwanda
ilipandisha ushuru huo na
kuwa dola 152 bila kujali
umbali, kwa kuwa kijiografia
haukuwa na msaada kwao .
Hata hivyo, taarifa zimeeleza
kuwa Tanzania haikulalamika
kwa ongezeko hilo la ushuru na
iliendelea kufanya biashara na
Rwanda kama inavyofanya na
nchi zingine zinazopitisha
mizigo yao katika Bandari ya
Dar es Salaam .
Hujuma kwa Tanzania
Katika mazingira yanayotafsiriwa
kuhujumu Bandari ya Dar es
Salaam , nchi hiyo mwanachama
mwenza wa Afrika Mashariki,
imepandisha ushuru tena hadi
dola 500 , mara hii ushuru huo
ukiwa kwa magari yanayopita
Bandari ya Dar es Salaam tu.
Ushuru huo kwa mujibu wa
taarifa hiyo, ulitangazwa ghafla
muda mfupi baada ya Kenya
kutangaza kuondoa vikwazo vya
barabara kwa magari ya mizigo
inayopita katika Bandari ya
Mombasa kwenda Kigali.
Mfanyabiashara aliyeathirika na
ushuru huo, alisema sasa ni
wazi kuna jaribio la Rwanda
kuonesha kuwa usafirishaji wa
mizigo kutoka Dar es Salaam
kwenda Kigali, umbali wa
kilometa 1, 350 , ni aghali kuliko
kusafirisha mizigo kutoka
Bandari ya Mombasa hadi
Kigali, umbali wa zaidi ya
kilometa 2, 700 .
Taarifa rasmi
Akizungumza na gazeti hili
jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Dk Charles Tizeba, alikiri Wizara
yake kupata taarifa za kupanda
kwa ushuru huo kupitia
wafanyabiashara, lakini hadi
sasa wizara hiyo haijapewa
taarifa rasmi na Rwanda.
Alisema juzi akiwa katika kikao
hicho cha mawaziri wa Afrika
Mashariki, Wanyarwanda
walikuwa wakilalamikia kiasi
cha ushuru kinachotozwa
nchini katika barabara kuwa ni
mkubwa ikilinganishwa na nchi
za Afrika Mashariki.
Alisema kutokana na
malalamiko hayo , alilazimika
kuwajibu kuwa ushuru huo ni
lazima utozwe kutokana na
vigezo vilivyowekwa na lengo
lake kubwa ni kulinda barabara .
“Kama Wizara hatujapata
taarifa rasmi, lakini tumepokea
malalamiko kutoka kwa
wafanyabiashara kuhusu
kutozwa ushuru huo mpya ,
tunachofanya sasa ni kuangalia
namna suala hili litakavyoathiri
usafirishaji na baada ya hapa ,
tutashauri wizara za fedha na
ujenzi hatua za kuchukua,”
alisisitiza.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dk Stergomena Tax
ambaye sasa ni Katibu Mtendaji
wa Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC ), alisema hatua hiyo ya
Rwanda kupandisha ushuru ni
ya kutengeneza ushindani usio
sawa.
Kwa mujibu wa Dk Tax , kwa
sasa Bandari ya Dar es Salaam
inafanya vizuri ikilinganishwa
na ya Mombasa na ndiyo maana
anaona ushuru huo ni wa
kuweka mazingira yasiyo sawa
ya ushindani kati ya Bandari ya
Dar es Salaam na ya Mombasa .
“Tangu Rwanda ilipojiunga na
Jumuiya ya Afrika Mashariki,
ilikuwa ikilalamikia vikwazo vya
Tanzania vya barabara , lakini
ukweli ni kwamba Tanzania na
Kenya zimekuwa zikijenga
barabara zake zenyewe, ndiyo
maana ni vema zitengeneze
mkakati wa kudhibiti matumizi
ya barabara hizo ili zikiharibika
kuwe na fedha za kuzikarabati, ”
alisema.
Suluhisho
Hata hivyo, Dk Tax alisisitiza
kuwa kabla ya kuondoka wizara
hiyo ya Afrika Mashariki , tayari
nchi za Jumuiya hiyo zilikuwa
na mkakati wa kuanza kutumia
kiwango kimoja cha uzito wa
magari kisichozidi tani 55, ili
kuhakikisha miundombinu ya
nchi hizo hususani barabara
haiharibiwi na uzito wa magari
hayo.
“Hili ndilo suluhisho la pekee
iwapo nchi zote za Afrika
Mashariki zitakuwa na kiwango
kimoja cha uzito , hata tozo za
ushuru zitakuwa sawa na
ushindani inaowaumiza
wafanyabiashara hautakuwapo, ”
alisisitiza.
Msemaji wa Chama cha Umoja
wa Wasafirishaji wa Malori
nchini ( TATOA) , Zacharia Hans-
Pope, alikiri kuwa na taarifa za
kupandishwa kwa ushuru huo
na hadi jana jioni magari ya
mizigo zaidi ya 200 yalikuwa
yamekwama Rusumo kutokana
na kushindwa kulipa tozo hiyo.
“Magari zaidi ya 200
yamekwama pale Rusumo kwa
kuwa hayana uwezo wa kulipa
tozo hiyo … ni kubwa mno , sisi
chama tunasubiri tamko la
Serikali ya Tanzania , kwanza
hatukuwa na taarifa kabisa juu
ya suala hili, ” alisisitiza.
Alisema ushuru huo utakuwa
‘mwiba’ kwa Bandari ya Dar es
Salaam kwa kuwa utaifanya
ionekane kuwa ya gharama
kusafirisha mizigo kwenda Kigali
jambo ambalo si la kweli.
Ni nchi za SADC pekee ndizo
zenye ushuru mmoja wa
barabara ambao ni dola 16 kwa
kilometa 100 za barabara , lakini
bado Jumuiya ya Afrika
Mashariki haijaweka kiwango
kimoja cha tozo hiyo.
CHANZO: HABARI LEO
SEPTEMBA 3, 2013

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑