Kazimoto apiga bao 2 Qatar

image

NEEMA imeanza kumjaa kiungo
wa zamani wa Simba, Mwinyi
Kazimoto , baada ya kupiga
mabao mawili safi akiwa na
timu yake mpya ya Al Markhiya
ya Qatar.
Kazimoto amefanikiwa kufunga
mabao mawili katika mechi tano
alizoichezea timu hiyo
inayoshiriki daraja la pili nchini
Qatar.
Pamoja na kufunga mabao hayo
mawili katika mechi tano za
kirafiki alizocheza, Kazimoto
amefanikiwa kupata namba ya
kudumu katika kikosi cha
kwanza .
Kocha wa zamani wa Simba ,
Hassan Afif , aliyemsaidia
Kazimoto kujiunga na timu hiyo
nchini Qatar, ameliambia
Championi Jumatatu kwamba
kocha wake kutoka nchini
Serbia amemhakikishia namba
katika kikosi cha kwanza .
“Kweli amefunga mabao mawili
katika mechi hizo tano,
walikuwa wamekwenda kuweka
kambi nchini Tunisia na sasa
wamesharejea hapa Doha tayari
kwa ajili ya ligi itakayoanza wiki
mbili zijazo.
“Kazimoto ameonyesha uwezo
mkubwa sana kwa kweli , mabao
aliyofunga ni mazuri .
Kilichomvutia zaidi kocha ni
kwamba, katika mechi zote tano,
hajacheza dakika 90 katika kila
mchezo, lakini amefanya vizuri.
“Wakati mwingine alianza au
kuingia katika kipindi cha pili ,
kocha alifanya hivyo kwa ajili ya
kujaribu wachezaji lakini
inaonekana kama
amejihakikishia namba katika
kikosi cha kwanza na kocha
ametaka aendelee na juhudi
hizo,” alisema Afif .
Akiyaelezea mabao ya Kazimoto ,
Afif alisema: “Sijayaona lakini
kocha kaniambia ni mazuri na
moja lilikuwa ni la shuti kali
nje ya eneo la kumi na nane .
Iimemfurahisha sana. ”
Kazimoto amejiunga na Al
Markhiya akitokea Simba
ambayo ameichezea kwa misimu
miwili, kabla ya hapo alikuwa
kiungo tegemeo wa JKT Ruvu .
Kazimoto ambaye amechipukia
kisoka mkoani Mwanza
alikozaliwa , anasifika kwa
kupiga mashuti makali pia pasi
za uhakika zinazozaa mabao na
amekuwa akifunga mabao kwa
mashuti ya mbali akiwa na
Simba pamoja na Taifa Stars.

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑