MAKOSA 10 WANAWAKE HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA

image

Kitanda kina kanuni zake. Kuna
makosa mengi hufanywa na
wanawake, vilevile yapo ambayo
wanaume huyafanya . Si sawa
kuyaacha yaendelee kuwepo kwa
sababu faragha ni hatua
muhimu katika ukamilishaji wa
kitu kinachoitwa penzi.
Uhusiano wa kimapenzi una
wigo mpana . Kuna mambo
mengi ambayo yakifanywa
huufanya mwili uwe na afya.
Hata hivyo, suala la faragha
halipaswi kusahaulika , kwa
maana ni chachandu
madhubuti.
Tendo la faragha lina nguvu
sana katika kuuweka hai
uhusiano. Wapo watu ambao
picha zilikuwa haziendi katika
maisha ya kawaida lakini kila
wakikutana kitandani, kila
mmoja alimvulia kofia
mwenzake.
Hii ina maana kuwa
inawezekana mwenzi wako
akawa dhaifu katika maeneo
mengine lakini ‘maujuzi ’ yake
faragha, yakakufanya uwe
mtulivu kwake.
Vivyo hivyo , nawe hakikisha
unampatia mwezi wako katika
eneo fulani ili hata akikufanyia
visa, basi uwe na ukurasa wako
ambao akiufikia ni lazima
akuvulie kofia. Faragha ni
uwanja huru ambao ambao
hudhaniwa ni mgumu lakini ni
rahisi sana .
Haihitaji msuli mkubwa wala
nguvu kama za samba .
Usidanganyike kwenda kutumia
madawa ya kuongeza nguvu
wala kwenda kwa waganga eti
ndiyo wakuboreshee mvuto
wako. Tuliza kichwa, soma
kitendo chenyewe halafu
hakikisha hufanyi makosa.
Katika makosa mengi ambayo
wanawake huyafanya wakiwa
faragha, ndani ya mada hii,
nimeyaunganisha na kuyafanya
yasomeke 10. Nikuhakikishie
kuwa ukiyaepuka na kufuata
mwongozo sahihi, utakuwa bora
sana.
Mambo mengi hayahitaji
taaluma, ni suala la
kuushirikisha ubongo ili uamue
kinachotakiwa. Mathalan;
kuzungumza na mwenzi wako
kumuuliza nini umfanyie ili
afurahie tendo au
kumwelewesha cha kufanya
aweze kukupatia , haihitaji
maarifa mengi au uwezo wa juu
kiakili.
Kujifanya unajua sana
husababisha wengi kuchemka.
Achana na tabia ya kuhisi wewe
umekamilika na kujidanganya
kwamba unafahamu kila
kinachotakiwa katika uwanja
mahsusi wa faragha .
Inakugharimu kiasi gani
kuzungumza naye ili akujuze
mahali hisia zake zilipolalia?
Yupo mwanamke ambaye tangu
anazaliwa mpaka anakua ,
amekariri kwamba ukiwa faragha
dawa ni kuzungusha ‘ bakuli’
mwanzo mwisho. Matokeo yake ,
anakutana na mwenzi wake ,
badala ya kusoma mahitaji
yake, yeye akili , nguvu na ujuzi
wake wote anauelekeza katika
nyonga tu. Mauno mtindo
mmoja.
Hajui kwamba pengine mwenzi
wake hapendi purukushani za
kupanda na kushuka.
Inapotokea wewe ni mtaalamu
wa kucheza juu ya msumari
(wana wa unyago mnaelewa),
dakika 90 hushushi mzigo chini ,
ukidhani unamfurahisha,
kumbe unageuka kero kwa
mwezio.
Inaweza kutokea umekariri kuwa
ukiwa katika utekelezaji wa
sanaa ya faragha lazima
uporomoshe mayowe. Japo ni
nzuri katika kupata mrejesho
(feedback ) wa tendo lenyewe
lakini si ajabu mwenzako
hafurahii hilo. Zungumza naye
tafadhali .
Hekima za tendo zinakataa
ububu, lazima muwe
mnaambiana mara kwa mara.
Kama siku hajakutendea haki ,
mweleze waziwazi kwamba
hajakufikisha. Ukimwacha
afanye anachotaka na
anachojisikia yeye, mwishowe
haitakuwa na msisimko kwako.
Tengeneza utofauti wa
makutano ya mbuzi na
binadamu. Maana beberu huwa
hajui maana ya kumwandaa
jike . Anapojisikia kupanda
anafanya hivyo na
anapotosheka anashuka. Wewe
na mwenzi wako hamna budi
kuwa na nidhamu . Hisia
ziheshimiwe.
Ikiwa mtatenda kwa
makubaliano, kila mmoja
akifuata maelekezo ya mwenzi
wake, akitilia mkazo yale
maeneo ambayo yametajwa
katika mazungumzo kwamba
ndiyo huleta raha, basi raha
huwa raha kweli . Zingatia
mambo 10 yafuatayo;
Itaendelea wiki ijayo

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑