WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA

image

Skendo ya mastaa mbalimbali
Bongo kutajwa katika biashara na
usafirishaji wa madawa ya kulevya
‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya
ambapo tayari majina ya wasanii
wawili wakubwa, Wema Isaac
Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond
Platinumz’ yametajwa huku
kinachowaponza kikijulikana.
Habari zinadai kuwa mastaa hao
wameanza kujutia tambo zao za
kutangaza utajiri walionao hivyo
kuibua maswali kuwa huenda wana
uhusiano na wafanyabiashara wa
dawa za kulevya ikiaminika ndiyo
njia ya haraka ya utajiri.
WEMA
Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema
kutangaza kununua nyumba,
magari ya kifahari na kutapanya
fedha ndiko kulikomponza na sasa
anatajwa na wengi vinywani mwao
juu ya kuhusika katika biashara
hiyo haramu.
Kuna madai kuwa bosi huyo wa
Endless Fame Productions
amehojiwa juu ya suala hilo lakini
meneja wake, Martin Kadinda
alikanusha uvumi huo.
DIAMOND
Wiki iliyopita, Diamond aligeuka
gumzo baada ya kuripotiwa
akihusishwa na biashara hiyo huku
ikidaiwa kuwa kinachomponza ni
utajiri alioupata ghafla.
Ilidaiwa kuwa kitendo cha
kutangaza kununua nyumba
takriban tano jijini Dar, kumiliki
kiasi cha Sh. bilioni moja kwenye
akaunti na kuendesha magari ya
kifahari ndivyo vilivyochangia watu
kugeuzia antena za runinga zao
kwake kutaka kujua ni matunda ya
muziki tu au kuna kingine.
Madai ya jina la Diamond kutajwa
katika saga hilo yalikwenda mbele
zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha
kusafiri mara nyingi nje ya nchi
huku akipiga picha na watu
wanaosemekana kujihusisha na
biashara hiyo nacho kilimponza.
Kwa upande wake, Diamond
alisema kuwa hakuna mtu asiyejua
namna anavyotafuta fedha kwa
jasho juani hivyo watu wakimuona
akila kivulini lazima wakumbuke
kuwa amechumia juani na hajui
chochote juu ya dawa hizo.

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑