HIVI NDIYO MFADHAIKO UNAVYOWATESA WATU BILA KUJIJUA

image

RIPOTI ya wiki imegundua kuwa
watu wengi nchini wanaugua
ugonjwa hatari wa mfadhaiko
(major depression) bila wao
kujijua.
Katika uchunguzi , ripoti hii
ilibaini kuwa ugonjwa wa
mfadhaiko umekuwa hautiliwi
maanani sana katika nchi
zinazoendelea ambako ndipo
watu wengi wamebainika kuwa
na ugonjwa huo tofauti na
mataifa yaliyokua kiuchumi.
Akizungumza katika mahojiano
na Ripoti ya Wiki, Dk. Richard
Marise wa jijini Dar alisema
ugonjwa wa mfadhaiko
hausababishwi na vimelea kama
magonjwa mengine , hivyo
kutojulikana sana na watu japo
kuwa huwa na madhara sawa
na magonjwa mengine .
“Mfadhaiko humpata mtu pindi
atakapopewa habari mbaya ,
kuachana na mwenza, ugumu
wa maisha , kuwaza kwa muda
mrefu, mateso (trauma ) na
kukata tamaa kwa kuugua
ugonjwa usiotibika mfano Kansa
au Ukimwi , ” alisema Dr.
Richard.
Akifafanua zaidi, mtaalamu
huyo alisema kuwa mfadhaiko
humfanya mtu kujitenga na
kutoshirikiana na watu
(isolation ), kutokuwa na furaha ,
kupungua kilo , kukosa hamu ya
kula, kuwa na hasira, kutojijali
na kushindwa kufanya tendo la
ndoa.
Matokeo mabaya ya mfadhaiko
ni pamoja na kupata magonjwa
ya moyo , kuugua vidonda vya
tumbo, kifo cha ghafla,
kujiingiza kwenye tabia
hatarishi kama matumizi ya
madawa ya kulevya na mwisho
kabisa kusababisha mtu kujiua
(suicide ).
“Mfadhaiko ni ugonjwa ambao
watu wengi wanao ukizingatia
kwamba wengi wetu ni maskini
na kila siku maisha yanazidi
kuwa magumu . Watu wengi
wanaishia kupatwa na msongo
wa mawazo na baadaye
mfadhaiko wakifikiria jinsi ya
kujikwamua,” alihitimisha Dr.
Richard.
Katika uchunguzi zaidi
uliofanywa na ripoti hii ,
iligundulika kuwa ugonjwa wa
mfadhaiko huchukuliwa kama
ugonjwa hatari katika nchi
zilizoendelea ambapo mtu
hupelekwa hospitali na
kutibiwa chini ya uangalizi wa
madaktari maalumu (psychiatric
specialists) mpaka pale
atakapopona huku dozi za
kupunguza makali ya ugonjwa
huo zikitumika tofauti na hali
ilivyo nchini.
“Ni wakati sasa tunatakiwa
kuutambua vizuri, madhara
yake ni makubwa pindi
mgonjwa anapokosa tiba
sahihi,” alisema daktari mmoja
ambaye hakupenda jina lake
liandikwe gazetini .
source:globalpublishers

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑