AUNTY EZEKIEL ACHANWA NA CHUPA CLUB, SOMA KISA HAPA NA TAZAMA PICHA ZA JERAHA NA AKIWA HOSPITALI

image

MWIGIZAJI wa sinema za
kibongo, Aunt Ezekiel Grayson
‘Gwantwa’ amenusurika
kupasuliwa paji la uso kwa chupa
baada ya kupigwa mkononi…
Usiku wa kuamkia Jumatatu, nje
ya Ukumbi wa Billicanas,
mwanamke aliyejulikana kwa jina
moja la Yvonne alimpiga Aunt
kwa chupa tupu ya bia na
kumpasua mkono wa kushoto.
Watu walioshuhudia tukio hilo
wamedai  kuwa, wakati Yvonne
anatekeleza ukatili huo, Aunt
alikuwa amesimama na marafiki
zake waliotajwa kwa jina moja
moja, Sajenti na Rehema.

image

image

“Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa
ikiendelea, Aunt, Rehema na
Sajenti walisimama nje, ghafla
alitokea Yvonne akiwa na chupa
mkononi, akailenga kwenye paji la
uso la mwenzake, bahati nzuri
Aunt aliiona na kukinga mkono,”
kilisema chanzo.
Kikaendelea: Vurugu kubwa
ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame
ili kushughulia suala hilo. Aunt
alikimbizwa Aga Khan, Yvonne
akapelekwa msobemsobe Kituo
cha Polisi cha Oysterbay, Dar
ambapo anashikiliwa.
Baada ya taarifa hizo, juzi
mchana, mwandishi wetu alifika
nyumbani kwa Aunt,
Mwananyamala na kumkuta
ambapo alikuwa na haya ya
kusema:
“Ishu ni kweli kama mlivyosikia,
lakini kule Agha Khan sikutibiwa,
niliambiwa daktari hayupo mpaka
saa mbili asubuhi na muda huo
ilikuwa saa kumi alfajiri.
“Ilibidi niende kutibiwa kwa
Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali
ambako nilishonwa nyuzi sita.”
mwandishi: Madai ya Yvonne ni
nini hasa?
Aunt: Yaani hata mimi sijui,
nilishangaa sana. Kwanza lengo
lake lilikuwa kunijeruhi kwenye
uso, lakini niliiona chupa
nikaikinga na mkono ndiyo maana
ikaniumiza.
mwandishi: Siku za nyuma
uliwahi kuingia kwenye mzozo na
Yvonne kwamba unamchukulia
mpenzi wake aitwaye Joff, siyo
kwamba ndiyo kisasi?
Aunt: Yale mambo yalipita, yeye
ana maisha yake na mimi nina
yangu.
-Risasi

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑