BASI UNAAMBIWA HII NDO KERO UTAYOKUTANA NAYO UKIFIKA DODOMA

image

image

Abiria wakiwa tayali wameshuka
katika Daladala baada ya kutoka
maeneo mbalimbali ya mji wa
Dodoma na kushushiwa
Barabarani baada ya kukuta
msongamano mkubwa katika
stand mpya iliyoanza kutumika
leo ya jamatini.(PICHA NA JOHN
BANDA, DODOMA)
WAKAZI wa manispaa ya Dodoma
wamelalamikia udogo wa Stand
kuu ya Daladala ya Jamatini na
kuitaka mamlaka nayohusika
kuliacha eneo la oil com
zilikokuwa zikipakilia abiria
wakati wa ujenzi wa stand hiyo
kuwa mbadala kutokana na wingi
wa magali.
Kauli hiyo ilitolewa wakati stendi
hiyo ilipoanza kufanya kazi kwa
mara ya kwanza jana ambapo
ilishuhudiwa wingi wa magali
hayo ya Abaria yakiingia na
kutoka huku kukiwa na
msongamano mkuwa kiasi cha
mengine kushushia abiria
Barabarani.
Mmoja wa Abiria wanaotumia
stand hiyo Winnie Binamu alisema
imejengwa vizuri lakini haikidhi
haja kutokana na kuwa ndogo
ukilinganisha na idadi kubwa ya
Daladala zilizopo hali
inayosababisha msongamano na
wengi kushusha abiria bila
utaratibu ilimradi wawahi
kupakia wengine.
Winnie aliongeza kuwa niafadhali
kama wahusika wangeiacha stand
iliyokuwa ikitumika kwa muda ya
oili com kuendelea kutumiwa na
baadhi ya magali ya njia nyingine
na mengine kupelekwa jamatini
kwa sababu kwa sasa watu ni
wengi tofauti na miaka ya nyuma.
Kwa upande wao madereva wa
Daladala hizi walisema stand
pamoja na uzuri haikidha
kutokana na njia moja kuwa na
magali zaidi ya 50 wakitolea
mfano njia ya Chang’ombe,
Mipango, UDOM, na kisasa zenye
abiria na Magali Mengi.
Mmoja wa madereva wa Daladala
zinazoelekea Ipagala Moses
Mamba alisema kwa sasa Dodoma
inawatu Wengi walioletelezwa na
vyuo pamaja na taasisi zilizo na
zisizo za kiserekali zinazoendelea
kuhamia mkoani hapa hivyo ni
vyema swala la stand hiyo
kuangaliwa upya na ikibidi
iwekwe ya ziada.
” Ona ndugu mwandishi leo ni
siku ya kwanza stand hii kuanza
kutumika lakini msongamano ni
kama unavyoona wengi
wanashushia abaria barabarani
kuanzia hapa yanapoingilia maka
karibu na kipita shoto[ Round
About] cha stand ya mabasi ya
mkoani je wakija wote kutokana
na tunavyojua itakuwaje?”, Alihoji
Mamba
Katibu wa Umoja wa wenye
Daladala [UWEDO] Peter Kabome
alisema Stendi hiyo haijawa Rasmi
ni kama inafanyiwa majaribio kwa
sababu haiwezekanai yakatakiwa
kuingizwa magali zaidi ya 300
kwenye eneo linalochukua magali
yasiyozidi 100.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya
Mipango Miji na Mazingira
manispaa Stephen Mwanga
alisema ameona msongamano huo
jinsi ulivyo mkubwa hivyo
atahakikisha anavihusisha vyombo
vinavyohusika kikiwemo
SAMATRA ili waweze kuona nini
cha kufanya ili walau kuliweka
sawa la staend hiyo

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑