ROBERT LEWANDOSKI: “KWANINI NILIKATAA KUJIUNGA NA MAN UNITED, REAL MADRID NA CHELSEA.’

image

Mshambuliaji wa Borussia
Dortmund Robert Lewandowski
amefunguka na kusema kwamba
amekataa kujiunga na vilabu vya
Manchester United, Chelsea na
Real Madrid ili aendelee kucheza
kwenye Bundesliga.
Baada ya tetesi za usajili
kumhusisha na vilabu kadhaa
barani ulaya, ikiwemo klabu hasimu
ya Dortmund – Bayern Munich,
Lewandowski sasa amesuluhisha
tofauti zake na Dortmund na
ameripotiwa kwamba tayari
ameongezea marat tatu mshahara
wake.a
Na mshambuliaji huyo mwenye
umri wa miaka 25 amezungumza na
kusema alifuatwa na vilabu kadhaa,
pamoja kuzungumza binafsi na
kocha Jose Mourinho.
Baada ya kufunga mabao manne
katika mchezo dhidi ya Real
Madrid katika mchezo wa raundi ya
kwanza wa nusu fainali ya
Champions League, Mpoland huyo
alipokea ujumbe wa simu kutoka
Mourinho: ‘Nataka uungane nami
katika klabu yoyote nitakayoenda.’
Lewandowski aliiambia The Sun:
‘Naweza kuthibitisha kwamba
niliongea na Mourinho. Tulikuwa
na mazungumzo mara kadhaa huko
nyuma. Nina namba yake ya simu
kwenye simu yangu. Ninahisi fahari
kuwa kocha mwenye jina kubwa
kama lake kunihitaji.
‘Mwaka mmoja uliopita niliongea
na Sir Alex Ferguson na kwa kweli
lilikuwa jambo kubwa na muhimu
kwangu.

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑