KIJANA ATIWA MBARONI KWA KUFANYA MAPENZI NA NG’OMBE HUKO KILIMANJARO….. ANADAI KILA AKITONGOZA HUKATALIWA

image

JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro
linamshikilia kijana mwenye umri
wa miaka 15 mwanafunzi wa kidato
cha pili katika shule ya sekondari
Kelamfua iliyopo wilayani Rombo
baada ya kukutwa akimwingilia
ndama wa ng’ombe.
Akithibitisha, Kamanda wa Polisi wa
mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3
mwaka huu saa 5:10 usiku
nyumbani kwao Kelamfua.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana
huyo ndiyo aliyemfumania kwa
kuwa alikuwa akimfuatilia kwa
muda mrefu na ndipo
alipomkamata.
Alisema kuwa kabla ya tukio hilo
kijana huyo aliwahi kukutwa
akifanya mapenzi na kuku na
kuanzia hapo mzazi wake huyo
akaanza kumfuatilia na hivyo
kumkamata akifanya mapenzi na
ng’ombe ambaye ni ndama.
Kamanda alisema kuwa baada ya
kukamatwa kijana huyo alifikishwa
kituo cha polisi na kuhojiwa
ambapo alikiri kufanya kitendo
hicho na kueleza kuwa amekuwa
akitafuta wasichana bila
mafanikio.
Aidha aliongeza kuwa kila
msichana anayemtakia neno la
mapenzi amekuwa akitaka fedha
nyingi wakati yeye ni mwanafunzi
hana uwezo wa kupata fedha.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana
huyo alishapata taarifa siku za
nyuma kuhusiana na tabia ya
kijana wake huyo na ndipo akaanza
kumfuatilia na kwa sasa
anashikiliwa na polisi uchunguzi
zaidi ukiendelea.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Up ↑